Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Tuesday, January 17, 2012

MWILI WA MBUNGE WA CHADEMA MAREHEMU REGIA MTEMA WAAGWA TAYARI KWA MAZISHI KESHO IFAKARA


Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.

Askari wa Bunge wakishusha Jeneza katikagari kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga.

Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga.

Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Willbload Slaa, akitoa salama za rambirambi.

Mwenyekiti wa CHADEMA, FreemanMbowe, akitoa salama za rambirambi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya Serikali.

Spika wa Bunge, Anne Makinda, akitoa wasifu wa mare hemu katika shughuli zake za kibunge na salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.

Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Slaa na mkewe wakiwa bize wakichati na simu 'sare sare' zinazofanana wakati wakiwa katika shuguli hiyo ya kuaga mwili wamarehemu. Haikuweza kufahamika mara mojawalikuwa bize katika suala lipi hasa.
Wengine pia walikuwa bize katika kunasa matukio ya shughuli hiyo, kama anavyoonekan mdada huyu, ambaye kivazi chake tu kilikuwa gumzo katika maaa kama hapo kwenye msiba, "utazani anaenda disco au Beach" walisikika baadhi ya watu wakinong'ona.

Baadhi ya watu waliohudhuria shughuli hiyo.

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.
 (SUFIANIMAFOTO

No comments: