ALIYEWAHI kuwa
mwenyekiti wa Chama cha soka Tanzania (FAT) sasa TFF ambaye ni
mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA), Muhidin Ndolanga jana aliponea kipigo toka kwa wa
Waumini wa Msikiti wa Kichangani, Magomeni Mapipa.
Tukio hilo lilitokea
mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa ambapo kama si askari wa
jeshi la polisi kumuokoa mambo yangekuwa mengine.
Kwa mujibu wa chanzo cha
kuaminika toka katika msikiti huo, ni kwamba Ndolanga ambaye ni
Mwenyekiti wa bodi ya msikiti huo, alikumbana na maswahibu hayo mara
baada ya kusoma taarifa ya kwa ajili ya kuwasilisha maamuzi yaliyofikiwa
na Bodi ya Udhamini iliyokutana kujadili mambo mbalimbali ya msikiti
huo.
Imeelezwa kwamba kwa
takribani miezi miwili viongozi wa msikiti huo wamekuwa kwenye mgogoro
mzito ambao umewahi kufika kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa
usuluhishi bila mafanikio.
Tukio hilo lilitokea
katika msikiti huo baada ya kumalizika kwa Swala ya Ijumaa ambapo
inadaiwa Ndolanga, alisimama kwa ajili ya kuwasilisha maamuzi
yaliyofikiwa na Bodi ya Udhamini iliyokutana kujadili mambo mbalimbali
ya msikiti huo.
Imeelezwa kuwa baada ya
kuisoma taarifa hiyo, waumini wa msikiti huo, walipinga taarifa hiyo na
kudai kuwa ni tofauti na matakwa ya waumini na ndipo waumini hao
walipopandwa na jazba na kutaka kumpiga makonde kiongozi huyo.
Hata hivyo Polisi waliwahi kumwondosha na kumkimbiza katika Kituo cha Polisi Magomeni.
Taarifa zinaongeza kuwa,
Baraza la Msikiti huo, lilimsimamisha Imamu Mkuu wa msikiti huo,Walid
Alhad na wasaidizi wake wawili, Japhary Mohamed na Murshad Athman kwa
tuhuma za ubadhirifu wa fedha.
No comments:
Post a Comment