Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia), akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba.(katikati),
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi, na
kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu.
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI
ya Multichoice Tanzania kupitia huduma ya DSTV imewataka wasanii
kupeleka kazi zao ili waweze kutambulika nje na ndani ya nchi.
Kauli
hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Meneja Masoko wa kampuni hiyo
Furaha Samalu wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba .
Alisema
kifurushi hicho mahususi kwa watanzania chenye chanieli zaidi ya 65
za kitaifa na kimataifa zikiwemo za Maisha Magic Swahili inayoonesha
filamu za Kiswahili, chaneli ya telemundo, chaneli ya nickelodeoni na
Disney junior zinazoonesha vipindi vya watoto.
Alitaja
chaneli nyingine zitakazopatikana kwenye kifurushi hicho ni Afrika
magic Epic Movie, Discovery world, CBS Action, CBS reality na CBS drama
pamoja na Select sport 1 na 2 kwa vipindi vya michezo.
Meneja
Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) Octoba 1,2014 jijini Dar es Salaam wakati wa
uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba.
“Uzinduzi
wa kifurushi hichi ni jambo la furaha na msisimko sana kwetu kuona kuwa
sasawatanzania wanaweza kupata kifurushi kinachokidhi mahitaji yao.
“Kila
wakati multichoice inafanya jitihada za kudumu namna ya kuwapa wateja
wetu uwanja mpana wa burudani kwa uwepo wa filamu , makala, habari,
vipindi vya watoto, muziki, vipindi vya dini na michezo,” alisema.
Aliongeza
kuwa kifurushi hicho kitagharimu kiasi cha shilingi 17,000 kwa mwezi
ambapo watakao jiunga watapata DSTV ikiwemo na gharama ya ufundi kwa
shilingi 99,000 kwa kipindi maalum.
Alifafanua
kuwa kifurushi hicho pia kitawapa fursa watanzania kuangalia Chaneli za
Super Sport select1 na 2 ambayo inatonesha ligi kuu ya Uingereza, kombe
la klabu bingwa ulaya, ligi kuu ya Hispania, ligi kuu ya Ujerumani
pamoja na riadha na ngumi.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akitoa ufafanuzi kuhusiana na kifurushi hicho.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi huo.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).
No comments:
Post a Comment