Daktari
kijana Brian Mushi wa Projeckt Inspire akionyesha upendo kwa mmoja wa
wazee wanaoishi kwenye kituo hicho kilichopo Msimbazi Centre mara baada
ya kumpima Presha wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
Na Mwandisi wetu
WAZEE
wanaoshi katika makazi ya Msimbazi Centre Jijini Dar es salaam karibu
na kanisa la Mtakatifu Maria wa Fatma, Msimbazi walipata faraja kubwa
baada ya kutembelewa na makundi matatu ya jamii.
Makundi
hayo ni pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini, Tushikamane
Pamoja Foundation na madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt
Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy.
Makundi hayo yalifika katika kituo hicho katika kuadhimisha siku ya wazee duniani.
Wakiwa
na lengo kuu la kuwafariji, kukagua afya zao na kuheshimu uwepo wao,
makundi hayo pia yaliwapa zawadi za vyandarua, sabuni za kufulia na
kuogea, pampers, Thermos Flask, vikombe vya chai, sahani za kulia,
vijiko, sukari, njugu mawe, Tshirts, viatu, nguo, vyombo vya kufanyia
usafi .
Pia walipiga picha za pamoja za ukumbusho.
Siku ya Wazee Duniani imetengwa kwa ajili ya kuweaenzi na pia kuwakumbuka kwa mambo waliyofanya kuendeleza kizazi cha wanadamu.
Dr. Brian Mushi wa Projeckt Inspire akimpima presha mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho.
Dr.
Brian Mushi wa Projeckt Inspire akichukua vipimo vya damu kwa ajili ya
kupima sukari kwa mmoja wa wazee wanaolelewa kwenye kituo hicho wakati
wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
Wafanyakazi
wa UNFPA kutoka kushoto ni Clementina Njau, Mike Mwakuvila na mdau
kutoka Tushikamane Pamoja Foundation wakionyesha upendo kwa mmoja wa
wazeee wanaoishi kwenye kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya
wazee duniani.
Dr.
Majaliwa Marwa kutoka UNFPA akikabidhi moja ya vyandarua walivyovitoa
kwenye kituo hicho kinacholelea wazee Msimbazi Centre wakati wa
maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
Sehemu ya msaada uliotolewa na makundi hayo.
Wafanyakazi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) hapa nchini wakiongozwa na mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA,
Sawiche Wamunza(kushoto), wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation pamoja
madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa
Inspire Healthy wakiwa kwenye picha ya pamoja na masista wanaowahudumia
wazee hao kwenye kituo hicho.
Wafanyakazi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) hapa nchini wakiongozwa na mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA,
Sawiche Wamunza(wa nne kushoto), wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation
pamoja madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya
mradi wa Inspire Healthy kwenye picha ya pamoja.
Wafanyakazi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) hapa nchini, wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation pamoja
madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa
Inspire Healthy kwenye picha ya pamoja na mmoja wa wazee wanaoishi
kituoni hapo.
No comments:
Post a Comment