Huduma ya Vodafone M-PESA yaongoza kimataifa
  Kampuni ya simu  za mkononi ya Vodacom  Tanzania imetajwa kuwa ni kampuni bora   kwa  utumaji wa fedha ulimwenguni kupitia huduma yake ya Vodafone M-Pesa.    
Taarifa hiyo ilitolewa  ilitolewa  wakati wa maonyesho ya  kwanza yanaohusu huduma za utumaji  pesa kwa  njia ya simu za mkononi yaliyofanyika Dubai tarehe 25 mwezi  huu.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare alisema  taarifa hiyo iliyopatikana  wakati wa maonyesho hayo imeipa faraja  kampuni yake .
 “Taarifa hiyo  inatambua mchango na viwango vya huduma zetu kwa  wateja pia  ,  alisema Mkurugenzi hiyo
Bw. Mare alisema kwamba  Kampuni hiyo haitabweteka kwa sababu  imepata heshima hiyo kubwa Ulimwenguni  kwa wa watoaji kwa huduma na  bidhaa bora na badala yake itaboresha huduma  zake. 
Hivi karibuni kampuni  hiyo ilishinda tunzo ya Chapa Bora kwa  Afrika Mashariki , ili kushinda  tunzo hiyo vigezo mbalimbali  huzingatiwa ikiwamo unora wa bidhaa.
Bw. Mare aliwashukuru  wateja wote wa Vodacom kwa uaminifu wao  na kuwahakikishia kwamba wataendelea  kuwapatia huduma bora wateja wake  ili waweze kukata kiu yao ya mawasiliano  na sanjari na huduma  mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.
“Tutaendelea kuwapatia  wateja wetu huduma bora ambazo zitakidhi  kiu yao ya mwasiliano lakini  katika hali ambayo wataimudu na yenye  manufaa kwao,” 
Vodafone M-PESA, ni  njia rahisi ya utumaji pesa kwa njia ya  simu za mkononi, njia hi ilizinduliwa  rasmi mwaka 2008, kwa hapa nchini  huduma hiyo imekubalika na inatumiwa  na Watanzania wengi.
Wateja wa Vodafone-MPESA  sasa wanaweza kulipia huduma  mbalimbali kama vile LUKU, bili za Dawasco,  kuongeza muda wa maongezi,  kutuma na kupokea fedha kwenda mtandao wowote  hapa nchini na kulipa ada  za wanafunzi.
Hadi sasa huduma hiyo  ina wateja zaidi ya milioni 5.4  waliojisajili sajiliwa katika huduma,  huku kila mwezi wateja wapya   500,000 wakisajiliwa.
Hivi sasa zaidi ya  shilingi bilioni mia sita 600 zimeshatumwa  kupitia mtandao huo huku  idadi ya mawa
 
 
No comments:
Post a Comment