Baadhi ya Wabunifu wa Mavazi  watakaoshiriki katika Swahili Fashion Week wakiwa katika picha ya  pamoja.
Jukwaa  la tatu la Swahili fashion Week linaanza leo katika viwanja vya  karimjee jijini Dar es salaam na kudumu kwa muda wa siku tatu hadi  tarehe 6 ya mwezi wa November 2010.
Katika  jukwaa la mwaka huu jumla ya wabunifu 24 kutoka nchi za Afrika hasa  zile zinazozungumza lugha ya Kiswahili wamejiandaa vya kutosha katika  kuonesha kazi zenye viwango vya kimataifa.
“Tunashukuru  kwani mipango yote inakwend kama tulivyopanga na tayari wabunifu wote  wamefika kwa ajili ya shoo kabambe ambapo itakuwa na tofauti kubwa  kulinganisha na zile zilizopita. Tayari wabunifu wote 24 kutoka Tanzania  na nchi za Pan Afrika wapo tayari kwa shoo ya mwaka, inayoandaliwa  nyumbani mwa Swahili Fashion Week.”  Alisema Mustafa Hassanali muandaaji  wa Swahili Fashion Week
“Kwa  mara nyingine tena tupo na Swahili Fashion Week 2010, na kusaidia  kukuza Sanaa ya ubunifu wa mavazi hapa nchini, pamoja na kuwakaribisha  wageni wetu ambao ni wabunifu wa kimataifa. Southern Sun inajivunia  kutokana na mchango wake inayotoa  kwa Sanaa ya ubunifu wa mavazi Afrika  na hii intupa fursa ya kuendelea kwa njia mbalimbali.” Alisema  meneja  mkuu wa southern sun Hotel Ndugu Adam fuller
Southern  Sun hotel imekuwa nyumba ya Swahili Fashion Week toka mwaka 2009.
Swahili Fashion Week  inafanyika kwa mwaka watatu  sasa na  itawashirikisha wabunifu 24 ambapo  kwa mujibu wa ratiba,  siku ya kwanza shoo  itapambwa na Manju Msita  (Tanzania),Sonu Sharma (Kenya),Shelina Ebrahim (Tanzania/Canada),United  Against Malaria (Tanzania Various),Farha Sultan (Tanzania),Tanzania  Mitindo House (Tanzania - Various), KemiKalikawe (Tanzania) na Asia  Idarous (Tanzania)
Kwa  upande wa tarehe tano, siku ya ijumaa mwanamitindo kutoka Tanzania  Jamila Vera Swai tfungua pazia akifuatiwa na Marinella Rodriguez  (Mozambique),Stella Atal (Uganda),Kooroo (Kenya),Zamda George  (Tanzania),Mafi Designs (Ethiopia),Moo Cow (Kenya),Robi Morro  (Tanzania),Made by Africa (Tanzania) na Asos Africa (UK)
Tarehe  sita November siku ya mwisho ya jukwaa la Swahili Fashion Week,  wabunifu wtakoonesha kazi zao ni pamoj na wabunifu wanane wanaochipukia  waliofanikiwa kuingia fainali kupitia shindano la wabunifu  wanaochipukia, Emerging Designers Competition (Tanzania -  Various),Gabriel Mollel (Tanzania),Khadija Mwanamboka  (Tanzania),KikoRomeo (Kenya), John Kaveke (Kenya), Chichia London  (Tanzania/UK), Ailinda Sawe (Tanzania)
“  Pamoja na kuwakaribisha wageni wetu ambao ni wabinifu wa mavazi , pia  Southern itatoa zawadi kwa gauni bora katika Swahili Fashion Week kwa  huu , lengo ni kusaidia kukuza Sanaa ya ubunifu wa mavazi” Aliongeza   Saphia Ngalapi, Swahili Fashion Week PR manager
 
 
No comments:
Post a Comment