Male Models waiting to audition at the model casting at the  Southern Sun Hotel,victoria martin mwanamitindo maarufu nchini Tanzania amepita katika mchujo huo ni kazi na umuhimu wake atauwakilisha katika Giraffe unique model 2010 kama jaji mwanamitindo.   
 
                                             Selected Female Models for SFW 2010Wajasirimali  zaidi ya 50 watajumiika pamoja katika kuuza  na kuonesha bidhaa za aina  mbalimbali wanzozizalisha katika maonesho  yanyojulikana kwa jina la  Swahili Fashion Week Shopping Festival, maonesho  yanayokwenda sambamba  na onesho kubwa la mavazi linalowakutanisha wabunifu wa  mavazi kutoka  nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiswahili.
Swahili Fashion Week Shopping Festival itafanyika kuazia   tarehe 4th hadi 6th ya mwezi wa November 2010  katika  bustani ya Karimjee, na kuwashirikisha wajasiriamali kutoka  Zanzibar na Tanga, Kirimanjaro, Mtwara na Dar es salaam.
“Hii ni mara ya kwanza kwa Swahili Fashion Week Shopping   Festival kufanyika, lengo ni kutoa fursa kwa watu wa aina mbalimbali  ambao  watafika katika fashion show waweze kupata ladha ya tofauti na  maonesho ya  mavazi kwa kuona na kununua bidhaa mbalimbali ambazo ni  adimu”. pia kuchangia  kukuza dhana ya kupenda bidhaa zinazozalishwa  Tanzania.  Alisema Hamis Omar, Afisa masoko na mauzo wa Swahili Fashion  Week.
Katika maonesho kutakuwepo na bidhaa kama vile nguo, mapambo  ya aina mbalimba, vifaa vya  mapishi, henna na vingine vingi. Maonesho  yatakuwa wazi kuanzia asubuhi hadi  jioni kwa muda wa siku  tatu,  yaani  tarehe 4, 5 na 6 ya mwezi huu kwa Novemba 2010.
“Wazo la kufanya maonesho haya limekuja kufuatia  tathimini  tulioipata mwaka jana, ambopo tuliona kwamba pamoja na kuwepo maonesho   yalifanywa na wabunifu wa mavazi ya kuonesha nguo zao,  ambapo  watu mbalimbali  waliofika katika maonesho walitaka   kununua, ndio maana tukaja na tukio hili ili watu wa aina mbalimbali  wawaeze  kufurahi na kupata vitu adimu.” Aliongezea Hamis Omar. 
 
 
No comments:
Post a Comment