Miss Earth aondoka na matumaini ya kushinda Philippines.
MWAKILISHI wa Tanzania katika   mashindano ya  Miss Earth 2010, Rose Shayo aliondoka nchini jana kwenda  Vietnam  huku  akiwa na matumaini makubwa ya kufanya vyema katika  mashindano hayo.
Akizungumza  kabla ya kuondoka,  Rose alisema kuwa amejiandaa viliyvyo chini ya  muandaaji ake, Maria  Sarungi wa Compass Communications and bila shaka  atafanya vyema katika  mashindano hayo.
Rose  amesema kuwa haendi kuwa  msindikizaji katika mashindano hayo na  atafanya kila aliwezalo ili kufanya  vyema kama ilivyokuwa  kwa Miriam  Odemba mwaka 2008 nchini Philippines.
“Najua  kuna kushinda na kushindwa,  mimi sitarajii kushindwa kutokana na  maandalizi yangu, nawaomba Watanzania  wanipe sapoti kubwa wakati wote  nikiwa kambini na siku ya mashindano,”  alisema Rose.
Maria  alisema kuwa, alisema  mrembo huyo amejiandaa vizuri kwakuwa mashindano  ya kumsaka mrembo huyo  yalifanyika mapema mwaka huu.
 
 
No comments:
Post a Comment