Haya ni baadhi ya maumivu na kutoamini baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ambako kulimpelekea mgombea kuzimia ...ni hatari jamani inauma sana
HATIMAYE Chama cha Mapinduzi (CCM)  kimefanikiwa kutwaa jimbo la Tarime ambalo lilikuwa likishikiliwa na  chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa miaka mitano,huku  mgombea wa CHADEMA, Mwita Mwikwabe akiangua kilio hadi kuzirai. Mgombea  huyo alizirai baada ya matokeo kuhesabiwa tena na kubaini kuwa  ameshindwa ,ambapo mgombea wa CCM, ambaye ni mtunzi wa vitabu, Nyabari  Nyangwine,amefanikiwa kushinda kwa tafauti ya kura 730.
Akitangaza  mataokeo hayo msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Tarime, Fedelis  Lumato,alisema kuwa Mgombea wa CCM,Nyambari Nyangwine ameshinda kwa kura  28,064 huku  mgombea wa Chadema Mwita Mwikwabe akipata kura 27334  ambapo aliyekuwa anatetea kiti hicho Charles Mwera wa CUF akiambulia  kura 7368.
Lumato alisema kuwa  mgombea wa NCCR-Mageuzi ,Peter Wangwe  amepata kura 7811,mgombea wa UDP, Mchungaji Jacob Mwita ameambulia kura  185 akifuatiwa na mgombea wa TLP ambaye ni mwandishi wa habari na  Mwanasheria Kichere Nyaronyo aliyepata kura 45 tu.
Aidha CCM  imefanikiwa kutwaa halmashauri hiyo baada ya kupata madiwani 17 dhidi ya  Chadema waliopata madiwani 12 na CUF wakiambulia kiti kimoja kutoka kwa  aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Mwera aliyepewa aliyepata kujifariji.
Kwa  upande wa matokeo ya Rais Mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, amepata kura  34930 sawa na asilimia 49  dhidi ya Mgombea wa Chadema 32470 sawa na  asilimia 46 huku akifuatiwa na mgombea wa CUF aliyepata kura 1804 na  mgombea wa APPT-Maendeleo Piter Kuga Maziray akiambulia kura 889sawa na  asilimia 1.3.
Asilimia 42.5 ya wapiga kura katika  jimbo la Tarime ambao walijitokeza kupiga kura katika jimbo lenye wapiga  kura 160867 ambapo waliojitokeza ni 70907 jambo ambalo msimamizi wa  jimbo hilo alisema inahitaji utafiti kwasababu katika miaka ya hivi  karibuni wapigakura wamezidi kukosa muamko.
Hata hivyo licha ya  kwamba CCM wameshinda shamrashamra zao ni za mashakamashaka  kwani watu  waliojitokeza kusherekea ni wachache walionekana hawajiamini kama   wameshinda jimbo hili ambalo wamefanya kazi ya ziada na ngumu na  hatimiye kufanikisha ushindi huo. Pamoja na zoezi hilo kumalizika hali  ilikuwa tete tangu usiku wa kuamkia jana baada ya milio ya mabomu na  risasi kusikika sehemu mbali mbali  hadi jana mchama ambapo polisi  walikuwa wanafanya kazi ya kutawanya makundi ya vijana wanadaiwa kuwa ni  wafuasi wa CHADEMA waliokuwa  wakiandama kupinga matokeo.
 
 
No comments:
Post a Comment