Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Saturday, March 5, 2011

UNIQUE MODELs WASHINE ILE MBAYA MISS UTALII

[5.jpg]

  Happy Andrew  Gumbo mshindi nambari moja wa bonanza la unique model 2010 na mshindi namba mbili Miss utalii 2010 

Mariam Rabii mshindi namba tatu wa Giraffe unique model 2010 /2011 na mshindi wa tatu miss utalii 2011

Vijana wa magese "unique models" Mariam Rabii na Happywitney Andrew Gumbo ambao dicovered by Don Magese katika gemu la mitindo wameonyesha uwezo wao katika shindano hilo siku ya jumamosi baada ya kushika nafasi ya pili na tatu.

"Nimefurahishwa na vijana wangu kuonyesha kuwa wanavipaji tofautitofauti Happy kashika nafasi ya pili na Mariam kashika nafasi ya tatu pia mariam alipata tuzo ya mwanamitindo bora ni faraja kwangu" alisema magese.

 

 unique model 2010/2011


 Asia dachi...bado yuko jikono tunamnoa kupambana tasnia ya mitindo na urembo ...comming soon!!


 TIPS; kuanzia j3 niko tyt sana watizamaji nawaacha na kijana wangu ALLY ataendelea kuwapa mambo matamu kwa takribani wiki mbili.  c u for minute......


United yaangukia pua, tena

Liverpool imeichapa Manchester United kwa mabao 3-1, katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Anfiled.
Dirk Kuyt alifunga mabao yote hayo matatu katika mchezo uliotwaliwa zaidi na Liverpool.
Mabao hayo yalifungwa katika dakika za 34, 39, na 65.
Bao pekee na la kufutia machozi lilifungwa na Havier Hernandez katika dakika ya 90.
United wanasalia kileleni wakiwa na pointi 60, huku Liverpool wakiisogelea Tottenham kwa kufikisha pointi 42, huku Spurs wakiwa na 47.


MAVAZI NA SEHEMU ZAKE

Kama kawaida huyu mama haoni aibu antishia kwa kunengua mitaani, watu wanasema kuwa alichelewa kazini.

Wapinzani wakabiliana na majeshi ya Libya


Wapinzani nchini Libya wamezuia jaribio la majeshi ya serikali ya kuuchukua tena mji wa Zawiya, kilomita 50 magharibi mwa mji wa Tripoli.
Libya
Wapinzani wa Libya
Kufuatia mapigano makali siku ya Jumamosi asubuhi, majeshi ya serikali yalilazimishwa kusogea nje ya mji, ingawa baadhi ya taarifa zinasema wamejipanga upya na huenda wakawa wanapanga mashambulizi mapya.
Idadi ya vifo haiko wazi.
Wakti huohuo, wapinzani wanaompinga Kanali Muammar Gaddafi wamechukua udhibiti wa mji wa bandari wa Lanuf, mashariki mwa Tripoli.
Waangalizi wanasema kwa ujumla ni vigumu kujua nani anadhibiti wapi, wakati mvutano wa kuitawala Libya ukiendelea.
Mjini Tripoli, kuna hali ya kujiamini miongoni mwa wanaoutii utawala, huku udhibiti ukionekana kuongezeka mjini Tripoli na maeneo mengine ya kati, kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyepo huko.
Lakini katika maeneo mengine, waandishi wa habari wanasema waandamanaji wana ari kubwa ya kuuondoa utawala wa Kanali Gaddafi.
Taarifa kutoka Zawiya zinasema mji huo umeshambuliwa kutoka upande wa mashariki na magharibi kutoka kwa wanajeshi wa serikali wenye silaha nzito.

Maafisa wa Uingereza waachiliwa Libya

Manuwari ya Jeshi la Uingereza
Manuwari ya Jeshi la Uingereza
Kundi moja la wanadiplomasia wa Uingereza, wakiwemo wanajeshi sita ambao wanaaminika kuwa maafisa wa kijasusi SAS, wameachiliwa huru siku mbili baada ya kuzuiliwa mjini Benghazi, Mashariki mwa Libya.
Maafisa hao wanaaminika kuondoka mjini humo kuelekea nchini Malta wakitumia manuwari ya kijeshi HMS cumberland.
Ripoti zinasema wanajeshi hao walikuwa na mwanadiplomasia mmoja ambaye alikuwa akijaribu kushaurianana viongozi wa upinzani nchini Libya.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema maafisa hao walikamatwa na wanajeshi waasi baada ya kuwasili mjini Benghazi, kwa helicopta siku ya Ijumaa iliopita.
kundi hilo lilikamatwa baada ya kuingia ndani ya majengo ya afisi za wizara ya kilimo, wakati maafisa wa ulinzi wa Libya, walipogundua kuwa walikuwa wamebeba silaha, risasi, maguruneti, ramani na hati za kusafiria za raia wa mataifa manne tofauti.
Wanajeshi waasi nchini Libya
Wanajeshi waasi nchini Libya
Walioshuhudia kisa hicho wanasema watu hao walikana kuwa walikuwa na silaha.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, William Haque, amesema, juhudi za wanadiplomasia hao za kushauriana na viongozi wa upinzani nchini Libya kuhusu ghasia zinazoendelea nchini humo zimeshindikana.
Hata hivyo Haque, amesema wamefanikiwa kutatua mzozo ulioibuka kati ya waasi hao na maafisa wake.
Bwana Haque, ameongeza kusema baada ya mashauriano na viongozi wa upinzani nchini Libya, watatuma kundi lingine ili kujaribu kukwamua mazungumzo kati yao.
Wakati huo huo Haque, amekariri kuwa Uingereza bado inaungana na jamii ya kimataifa kumtaka kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, kuitikia wito wa raia wa nchi hiyo na kuondoka madarakani.


MASHINDANO YA TAIFA YA NGUMI YAMALIZIKA LEO

Baadhi ya Mashabiki wa Mkoa wa Ilala Wakimshangilia bondia wao Mussa Mohamed aliewawakilisha vema mwanzo mpaka mwisho wa mashindano hayo na kuiletea medali ya SHABA katikati ni timu meneja wa Mkoa huo  

SIMBA YANGA HAKUNA MBABE UWANJA WA TAIFA WATOKA 1-1

        ZUHRA MODEL


ONYESHO LA MAVAZI LA MUSTAFAH
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiRJXOTo3neaBuhLX6jdfXCo91T36OAUdxAXsKcOir4-NgYFHSu4KCheQRKGMYwyIXgYJm2lBhEuG2lc0T_ANNVobwfBgek0z3JCum0HCArY8QU1KEfNscsESJ7Uu0c4xMrfGTBbGkQzc/s1600/5.jpghttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihDhmf3KR3UebkJEy3R__qiQO2v8JSGZFs2dkEOd5vAFwio2J5T-tq6HSikNQHao1EzciqGc88JpykYEvY82X14fGwFJkYx1PiMteQVkOWQypGtKJ8ar5Yi-P5ZCtpTgx6bvejJEAK2CY/s1600/9.jpghttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg5rnbr_f90JsanQC8mbEgbRmVyUvYaVROA6yTvA5HpFl2tvFdXMDy61ja5SVKjvKlWOd_2iWxipoxrFZShW0gFyGOWiN74cQmVCkY05mT0TyY12U_C3YNQXkVMqday8RGWGT1t4zq36mQ/s1600/6.jpg
Sho hii ilifanyika jana jijini Dar

POZI LA WIKI

No comments: