Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, March 2, 2011

SITTA AICHANA SERIKALI


 Samuel Sitta amesema hasara ambazo taifa limepata kutokana na mikataba mibovu ni matokeo ya kasoro zilizopo katika mfumo wa utoaji wa elimu nchini.Sitta alisema hayo juzi usiku kwenye Sherehe za Maadhimisho ya miaka 10 ya Shirika la HakiElimu zilizofanyika jijini Dar es Salaam.Alisema kasoro hizo zimesababisha mfumo huo wa elimu nchini kuzalisha watendaji mafisadi, wasiokuwa na maadili katika utendaji.

Sitta alisema sekta ya elimu ni kama imepewa kisogo, kiasi kwamba hakuna uwiano wa kiutendaji wa watu wanaohitimu mafunzo mbalimbali ikilinganishwa na vyeti vyao vinavyoonyesha kwamba walifanya vizuri darasani.

"Tumeshuhudia miaka 10 iliyopita, serikali imeingia hasara kutokana na baadhi ya viongozi kukosa uadilifu, wakaliingizia hasara taifa kwa kusaini mikataba feki," alisema Sitta na kuongeza:"... Hayo yote ni kwa sababu ya kuipa kisogo sekta ya elimu. Hii inatoa viongozi

 MAHAKAMA YA NDIZI YAVURUGWA

Soko la ndizi na mitumba maeneo ya manzese limevunjwa rasmi kwa kusambaratishwa ile mbaya.

 

CHELSEA YAICHABANGA UNITED

Chelsea imeichapa Manchester United mabao 2-1 kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Lampard
Frank Lampard
United ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Chelsea kwa mkwaju mkali ulioachiwa na Wayne Rooney katika dakika ya 29.
David Luiz wa Chelsea alisawazisha bao hilo katika dakika ya 54 kwa shuti kali.
Dakika kumi kabla ya kumalizika kwa mchezo Frank Lampard alifunga bao la ushindi la Chelsea kwa mkwaju wa penati, baada ya beki wa United Chris Smalling kufanya makosa ndani ya eneo la hatari.
Nemanja Vidic alipewa kadi yekundu baada ya kumuangusha Ramirez nje kidogo ya eneo la hatari.
Ushindi wa Chelsea umeipeleka hadi katika nafasi na nne ikiwa na pointi 48.
Manchester United imesalia na pointi 60, nne zaidi ya Arsenal iliyopo nafasi ya pili, ikiwa na mchezo mmoja zaidi.

Milan Fashion Week Round Up

Milan Fashion Week is for the bigwigs – the Guccis, Armanis, Versaces and Pradas. This is the ramp that hosts the major league designers, the ones that manage to re-invent elegance every season. 
Spring/Summer 2011 was no different. While Marni, Jil Sander and Fendi played with texture and fabric, Donatella Versace re-introduced the late Gianni’s favourite –baroqueon most of the outfits. Gucci’s Frida Giannini brought back late 1970s glamour along with high-octane make-up and fur; both real and fake.

Still going with the Mad Men theme, Bottega Veneta showed feminine suiting and Etro stuck to its iconic collage formula with lacquered paisley prints, and splashes of sequins.

With Paris Fashion Week 2011 coming up, the final round of international fashion weeks has already commenced. But before you relax – don’t forget our Indian fashion shows as Lakme India Fashion Week kick-starts on 11th March.





Mkuu wa Wilaya ya Monduli Bw.Jowika Kasunga pamoja na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba kulia wakifunua jiwe la msingi kuashiria makabidhiano rasmi ya jengo lenye madarasa mawili yaliyojengwa kwa msaada wa Vodacom Foundation katika shule ya Sekondary ya wasichana ya Irkisongo iliyopo wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kwa thamani ya shilingi Milioni 30.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondary ya wasichana ya Irkisongo iliyopo wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Happiness Nyange kulia akimwelezea jambo Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba mara baada ya kukabidhi msaada wa jengo lenye madarasa mawili yenye thamani ya shilingi Milioni 30,yaliyojengwa na Vodacom Foundation.

Mkurugenzi mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akipongezwa na wanafunzi wa shule ya Sekondary ya Irkisongo iliyopo wilaya ya Monduli Mkoani Arusha baada ya Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom kukabidhi msaada wa Jengo lenye madarasa mawili yenye thamani ya shilingi Milioni 30.
 

Mbunge aliyevaa herini afukuzwa bungeni Kenya

Mbunge mmoja nchini Kenya amefukuzwa nje ya bunge kwa kuvaa mavazi yasiyo na heshima.
Ramani ya Kenya
Mbunge huyo wa jimbo moja mjini Nairobi,Gidion Mbuvi,alifukuzwa kwenye kikao cha jana kwa kuvaa miwani ya jua na herini ndogo za mawe yenye thamani.
Naibu spika wa bunge, Farah Maalim, alisema namna bwana Mbuvi alivovaa haionyeshi heshima kwa bunge,ambalo halijawahi kuwa na mbunge mwanamume aliyevaa hereni.

Naibu spika wa bunge alishtumiwa na wafuasi wa Mbuvi kwa kukosa uvumilivu.
Mbuvi anajulikana kama Sonko -- jina ambalo kwa lugha ya mtaani linamaanisha mtu tajiri anayeishi maisha ya kifahari.


WAREMBO WETU
Haya picha ndio hizo jamani toka last year TOKA DUKA LA TRUWORTHS

 mrembo wa wiki
Tami Chynn

Tami Chynn (born Tammar Anika Chin) is a singer, songwriter and dancer from Kingston, Jamaica. Tami Chynn (born 14 June 1984) was born in Kingston, Jamaica. Her father, Richard Chin, is of Chinese descent with Cherokee ancestry and her mother, Christine Chin is Afro-Jamaican and British. Her parents were in a band called The Carnations and her younger sister, Tessanne Chin, is also a reggae fusion singer and former member of the group 'Mile High'.  
Tami grew up in the parish of St. Andrew and attended St. Peter and Paul Preparatory School. She later attended Campion College in St. Andrew, Jamaica. In 1998, at age 14, she moved to Leamington Spa, UK where she spent three years studying the performing arts and in 2001, at age 17, moved back to Jamaica where she worked on her music career and recorded her first single "Rock U". -Wikipedia.org



Baadhi ya wadau wa Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa BASATA wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kula kiapo cha kupambana na rushwa, uvivu na kutokuwajibika.Kiapo hicho kiliongozwa na Msanii maarufu wa muziki wa falsafa,Vitalii Maembe aka Sumu ya Teja.
Wadau wa Jukwaa la Sanaa mapema wiki hii wamekula kiapo cha kupambana na rushwa pia dhuruma nchini huku wito ukitolewa kwa wasanii kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya matatizo hayo ambayo kwa sasa yanatajwa kuwa kikwazo katika kuleta maendeleo ya mtanzania.

Akiwasilisha mada kwenye Jukwaa hilo linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Juu ya Wasanii na Ukombozi wa Jamii,Msanii Vitali Maembe maarufu kama Sumu ya Teja alisema kwamba,sanaa ni chombo kilichoshushwa na Mungu kwa ajili ya kuikomboa jamii dhidi ya makucha mbalimbali ikiwemo rushwa na ufisadi hivyo wadau wa sanaa hawana budi kuitumia katika kuikomboa jamii.

“Kama kuna watu watapewa adhabu na Mungu kwa kutotimiza wajibu wao ipasavyo basi ni wasanii.Mungu ametupa sanaa ambacho ni chombo chenye nguvu katika kuikomboa jamii lakini badala ya kuitumia kwa kazi hiyo,tumeigeuza chombo cha starehe, kujizolea umaarufu na kupatia wanawake” alilalamika Vitali Maembe.

Aliongeza kwamba,yeye katika kazi zake za sanaa hataacha kuimba ukweli na matatizo halisi yanayoigusa jamii ingawa kuna watu wanachukizwa na msimamo huo na kwamba anaamini ameingia kwenye tasnia hii kuikomboa jamii na wajibu wa suala hilo ni wa msanii yeyote.

“Kuna watu wanachukizwa sana na mimi kuimba ukweli na matatizo yanayoikumba jamii,mimi sitaacha kufanya hivyo hata nikitishiwa na nyimbo zangu kuzuiwa kupigwa.Sanaa imegeuzwa chombo cha starehe na kutukuza anasa wakati jamii inateketea” aliongea kwa uchungu Maembe huku akiimba nyimbo zenye ujumbe mzito kama Afrika shilingi tano,sumu ya teja na nyingine nyingi.\

No comments: