Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Monday, February 28, 2011

NH.CHEYO ANAPENDA KUBANJUKA..!!


Mbunge wa UDP Bwana John cheyo inasemekana anaupenda sana wimbo wa DNA uitwao "banjuka".

  Cheyo wakati akihojiwa na redio moja hapa nchini alipoulizwa je anapenda muziki gani alitoa kauli ya kuduwaza wengi kuwa anapenda wimbo mmoja tu wa banjuka.

 

Waziri mkuu wa Tunisia ajiuzulu

Tunisia

Waziri mkuu wa Tunisia Mohammed Ghannouchi ametangaza kupitia televisheni ya taifa kuwa anajiuzulu- matakwa muhimu kutoka kwa waandamanaji.
 Alikuwa akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Tunis, baada ya kutoa hotuba ndefu akijitetea wakati alipokuwa madarakani
 Bw Ghannouchi anaonekana kuwa karibu sana na aliyekuwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali, aliyeondoshwa madarakani mwezi uliopita.

Bw Ghannouchi, mwenye umri wa miaka 69, amekuwa chini ya uongozi wa Bw Ben Ali tangu mwaka 1989.

Alisema, " Baada ya kutafakari kwa zaidi ya wiki moja, nikaanza kushawishika, na familia yangu iliniunga mkono, na hivyo kuamua kujiuzulu. Si kwamba nakimbia majukumu yangu; nimekuwa nikitimiza wajibu wangu tangu Januari 14

Misri yamzuia Bw Mubarak kusafiri


Bw Hosni Mubarak
Mwendesha mashtaka wa Misri ametoa hati ya kumzuia Rais aliyeondoka Hosni Mubarak kusafiri pamoja na familia yake.
Msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka alisema amri hiyo pia inapiga tanji fedha na mali zao.
Bw Mubarak aling'atuka Februari 11, baada ya kukaa madarakani kwa takriban miaka 30, kufuatia kuibuka maandamano yaliyofanywa na umma ukimpinga.
Inaarifiwa kuwa afya yake ni duni, akiishi kwenye nyumba yake ya kifahari huko Sharm el-Sheikh, lakini hajaonekana wala kusikika hadharani tangu alipoachia madaraka.
Alikabidhi uongozi wake kwa jeshi, ambapo iliteua serikali ya mpito itakayoandaa katiba mpya na uchaguzi pia.
Shirika la habari Reuters limeripoti kuwa ofisi ya mwendesha mashtaka alisema kizuizi hicho cha kusafiri na kupiga tanji mali zake ilitolewa wakati malalamiko yalipotolewa- ambapo haijfafanuliwa- dhidi ya familia ya Bw Mubarak wanachunguzwa.
Misri tayari imeziomba serikali kadhaa kupiga tanji mali za familia ya Bw Mubarak nje ya nchi.
Waandamanaji pamoja na wanaopinga ufisadi wamekuwa wakishinikiza mali za familia ya Bw Mubarak zichunguzwe, ambayo inakadiriwa kuwa kati ya dola za kimarekani bilioni moja hadi bilioni 70.
Hata hivyo, mwakilishi wa kisheria wa Bw Mubarak amekanusha taarifa kuwa aliyekuwa Rais alijilimbikizia mali akiwa madarakani.

 ARSENAL YALAMBWA 2-0

 Birmingham City imeshangaza wengi kwa kuichapa Arsenal 2-1 katika fainali ya Kombe la Carling.

Martins
Obafemi Martins baada ya kupachika bao la ushindi
Arsenal, waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya ushindi katika mchezo huo kwenye uwanja wa Wembley, walishindwa kutumia fainali hii kumaliza ukame wa vikombe katika klabu hiyo.
Nicola Zigic wa Birmingham aliandika bao la kwanza katika dakika ya 28, kufuatia mpira wa kona kupigwa.
Wenger
Arsene Wenger
Nahodha wa Arsenal katika mchezo huo Robin Van Persie akiongoza kwa mifano, alisawazisha bao hilo dakika sita kabla ya mapumziko.
Arsenal waliendelea kulisakama lango la City, lakini kipa Ben Foster alisimama imara hasa kwa kuzuia mikwaju ya Samir Nasri na Niklas Bendtner.
Mambo yalibadilika wakati mashabiki wakidhani huenda mchezo ukaenda katika dakika za nyongeza.
City
Alex McLeish, kocha wa City
Bao la ushindi la City lilipatikana katika dakika ya 89 baada ya kipa wa Arsenal Wojsiech Szczesny na beki wake Laurent Koscielny kujichanganya na kumpa nafasi Obafemi Martins kufunga bao aliloliita jepesi zaidi maishani mwake.
Ushindi huu unaipa nafasi City kucheza Ulaya msimu ujao. Mara ya mwisho Birmingham kushinda ushindi kama huu ilikuwa mwaka 1963.
Mara ya mwisho kwa Arsenal kunyakua kombe muhimu, ilikuwa mwaka 2005.

 
KIM KARDASHIAN AFURAIA KUPIGA PICHA ZA UTUPU
Mwanamitindo maarufu duniani kim kardashiani ameingia lawamani baada ya kupiga picha akiwa mtupu kwaajili ya gazeti la W,Aidha kim amefurahishwa na kitendo hiko kwakua kimemuongezea usuper-staa zaidi.


 ELIZABETH NA KELVIN WAFUNGA NDO

Mshindi wa dola 200,000 za Big Brother Africa 4-The revolution iliyofanyika mwaka 2009,Kelvin Chuwang Pam aka Shemeji toka pande za Jos Plateau-Nigeria amefunga ndoa na housemate mwenzake wa Big Brother Africa 2009 toka TZ,Elizabeth Gupta kwenye sherehe ya harusi iliyofanyika jijini Lagos-Nigeria.
Kelin na Elizabeth wameweka historia ya kuwa housemates wa kwanza walioshiriki Big Brother Africa kufunga ndoa,acha engine walioishia kuchakachuana kwenye jumba hilo....Big Up,tunawatakia ndoa njema

 WATANZANIA WACHEMSHA MBIO ZA MARATHON 2011
Washiriki wa mbio hizo wakianza kutimua mbio baada ya kuanzishwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Moshi.

Jaribio la mapinduzi lazimwa Congo

Habari kutoka Kinshasa zinaeleza kuwa watu saba wameuawa baada ya kufanya jaribio la kumpindua Rais Joseph Kabila katika makazi yake.
Watu hao waliuawa na walinzi wa Rais Kabila, kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo.
Mwandishi wetu Lubunga Bya'Ombe akiwa Kinshasa amethibitisha kumetokea taarifa hizo. Hata hivyo watu waliohusika bado hawajajulikana.
Taarifa zaidi tutawaletea kadri zitakavyokuwa zikipatikana.


IZ IT INDIAN GIRLS ARE COLD?

Inasemekana hivyo ila mimi sijawahi kupruvu hivyo,tungependa kupata maoni tokwa kwa wadau


 NYUMBA YATEKEKETEA MOTO MTONI KWA AZIZ ALLY HUSIKU WA JANA
Gari la zima moto likiwa katika eneo la tukio wakati ilipotokea ajari ya moto ambabpo chanzo chanzo cha moto kilianzia kwenye salon ya kiume.


Saturday, February 26, 2011

SHILOLE ATANGAZA VITA NA WALA VIRINGI

Msanii chipukizi wa filamu Zena mohamed "shilole" amethubutu kudai kwa kukieleza moja vyombo vya habari kuwa hashobokei mapapaa"wala viringi".
Licha ya binti huyo kuwa na shepu ya kuwastua wanaume wengi wenye fedha zao hapa mjini shilole kadai sio limbukeni wa kushobokea mafweza ana true love kwa muhusika wake.
Hebu tufuatilie kwa kina kama miezi kadhaa atadumisha hiyo kauli yake kwani kujigamba huko kumewakwaza sana wakwale hao.

 UN yamwekea vikwazo Gaddafi
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura - na kupita bila kupingwa - ya kuuwekea vikwazo utawala wa Muammar Gaddafi kutokana na hatua yake ya kutaka kuzima maandamano.
UN
Wajumbe wa UN wakipiga kura ya vikwazo kwa Gaddafi
Baraza hilo limeunga mkono kuweka vikwazo vya silaha na kupiga tanji amana, huku wakifikisha suala hilo katika Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinaadamu.
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kiongozi huyo wa Libya aondoke madarakani na kuondoka nchini humo.
Hata hivyo bado anadhibiti mji wa Tripoli, lakini upande wa mashariki wa nchi unashikiliwa na waadamanaji.
Majadiliano ya kuunda serikali ya mpito ya wanaompinga Gaddafi inaarifiwa yanafanyika.
Mustafa Abdel-Jalil, aliyejiuzulu uwaziri wa sheria kwa kupinga matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji amesema tume yenye raia na wanajeshi itaandaa uchaguzi katika kipindi cha miezi mitatu, limekaririwa gazeti binafsi Quryna.
Libya
Waandamanaji Benghazi
Mabalozi wa Libya nchini Marekani na katika Umoja wa Mataifa wameunga mkono mpango huo, ambao unajadiliwa katika mji wa mashariki unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi.
Umoja wa Mataifa (UN) unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wamekufa, wakati utawala wa Kanali Gaddafi ukijitahidi kuzima vuguvugu la mabadiliko lililodumu kwa siku kumi.
Hii ni mara ya pili tu kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufikisha nchi katika ICC, na ni kwa mara ya kwanza kura kama hiyo kupita bila kupingwa.


 WANAJESHI WATOA KICHAPO GONGO LA MBOTO
    kichapo hiko kilitolewa na wanajrshi mida ya sita usiku kwa kuwadunda raia kwa mabuti,makofi na virungu,imeripotiw a watu 8 kujerhiwa na mkong"oto huo madhubuti.

    Yapata takriban tisa baada ya Dar es Salaam kutikiswa na milipuko ya mabomu na makombora katika kikosi cha Jeshi cha 511 ambacho ni Ghala Kuu la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Gongo la Mboto, askari zaidi ya 30 wa kikosi hicho wanadaiwa kupiga raia.
Askari hao inadaiwa waliwapiga raia hao usiku wa kuamkia jana kwa madai ya kulipiza kisasi baada ya mwenzao kupigwa na raia wa eneo hilo.




 WALIBYA WAJIAMDAA KWA VITA DHIDI YA GADDAFI
Watu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli wanajiandaa kwa mapambano zaidi, baada ya kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi kusema atafungua maghala ya silaha kwa ajili ya wanaomuunga mkono.
Gaddafi
Kanali Gaddafi
Uondoaji wa maelfu ya wafanyakazi wa kigeni unaendelea kwa njia ya anga, bahari na barabara, lakini wengine bado wamekwama.
Marekani imezuia matumizi yoyote ya fedha na amana za Kanali Gaddafi na baadhi ya watu wake wa karibu.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wamekufa katika mzozo wa kisiasa wa siku 10.
Siku ya Ijumaa, waandamanaji wanaopinga serikali mjini Tripoli wameshambuliwa kwa nguvu na bunduki.
Shirika la habari la AP limesema, limeelezwa kuwa serikali ya Kanali Gaddafi inawapa silaha raia wanaoiunga mkono ili kuweka vizuizi mjini Tripoli na kuwabana waandamanaji.
Wakazi ambao wamezungumza na AP kwa njia ya simu siku ya Jumamosi, wameripoti kuwa magari ya raia wanaomuunga mkono Kanali Gaddafi yanafanya doria mitaani.


BONGO FLAVA FC YAILAMBA BONGO MOVIE FC 2-0 

   Kikosi cha Bongo flava fc
Kikosi cha Bongo MOVIE FC

Meya wa Manispaa ya Ilala Jelly Slaa akisalimiana na 'Muuaji' wa Bongo Movie H.Baba.




 

WASHIRIKI WA MISS UTALII WANGOJEA SIKU

Jumla ya warembo 45 wanaotaraji kushiriki katika kinyang'anyiro cha kumsaka miss utalii Tanzania mwishoni mwa wiki ijayo tarehe 5 march 2011,wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Dar es salaam baada ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari na Rais wa Miss Utalii Tanzania Gideon Chipungahelo. Mshindi wa shindano hilo anataraji kuondoka na mkataba wenye thamani ya shilingi milioni 150 ambao utajumuisha kusomeshwa chuo kikuu, gari, fedha za kujikimu na naulishindano hilo litafanyika wilayani Bagamoyo jumamosi ijayo.



MISS TZ AENDA CHINA LEO
Mrembo mwenye mvuto na mshindi wa taji la Miss Tanzania 2010/2011Geneviev Emanuel  ameondokas leo kwa ndege kuelekea china kwa takribani wiki tatu.

TUNISIA WAANZA MAANDAMANO UPYA Polisi wamewatawanya waandamanaji katika mji mkuu wa Tunis siku ya Ijumaa wakidai kujiuzulu kwa Mohammed Ghannouchi, ambaye amekuwa akiongoza nchi hiyo baada ya Ben Ali kuikimbia Tunisia mapema mwaka huu.

Waandamanaji nchini Tunisia
Waandamanaji nchini Tunisia
Ulikuwa umati mkubwa zaidi tangu Rais Ben Ali kuikimbilia Saudi Arabia mwezi uliopita.
Ben Ali alikuwa Rais wa Tunisia kwa kipindi cha miaka 23 na alitimuliwa baada ya wiki kadhaa za maandamano.
Bw Ghannouchi na serikali yake ya mpito walitangaza wataanda uchaguzi utaofanyika mwezi wa Julai.
Lakini waandamanaji wanaonekana kutoridhishwa na walikuwa wakiimba mitaani 'Ghannouchi ondoka.'
Polisi walifyatua risasi za ilani na mabomu ya kutoa machozi karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Walioshuduia tukio hilo wanasema mtu mmoja tu ndiye aliyejeruhiwa miongoni mwa waandamanaji takriban 100,000.
Bw Ghannouchi aliwahi kufanya kazi katika serikali ya Ben Ali tangu mwaka 1999.


PICHA ILIOMTIA RIHANNA MATATANI 

Mwili wa Rihaana ilipigwa na chriss beez enzi za uhai wa penzi lao


 KESI YA MAGUFULI WASHTAKIWA WAGOMA
John MagufuliHATIMAYE raia 34 wa kigeni wanaokabiliwa na kesi ya uvuvi haramu kwenye ukanda wa Bahari ya Hindi maarufu “Kesi ya Samaki wa Magufuli’ jana waligeuka mbogo na kumuomba Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Radhia Sheikh, ajitoe kusikiliza kesi hiyo kwa sababu hawana imani naye.
Ombi hilo liliwasilishwa na mawakili wa washtakiwa hao, John Mapinduzi na Ibrahimu Bendera, mahakamani hapo ikiwa ni saa chache baada ya jaji huyo kutoa uamuzi wa kuwanyima dhamana licha ya kifungu cha 148 (6) na (7) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, makosa yanayowakabili washtakiwa kuwa na dhamana.
Sababu ya jaji huyo kuwanyima dhamana ni kwamba mazingira ya kesi hiyo washtakiwa wakipewa dhamana wanaweza wakaruka.
“Wateja wangu wamenieleza kuwa hawana kabisa imani na wewe na wanaomba ujitoe uongozi wa mahakama umpange jaji mwingine kwa sababu wanaamini dhamana ni haki yao.
“Wateja wangu wamenieleza kwamba kilichowashtua zaidi ni kwamba mapema mwaka jana jaji wa mahakama hii, Njegafibili Mwaikugile, alishatoa masharti ya dhamana kwa wateja wangu na ambapo wateja wangu walikimbilia Mahakama ya Rufani na jopo la majaji wa rufani watatu waliokuwa wakiongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Agustino Ramadhan liliamuru ombi hilo la washtakiwa la kutaka wapatiwe waliwasilishe Mahakama Kuu na mahakama hiyo isikilize ombi hilo.
“Mimi pamoja na wateja wangu tulitekeleza amri ya Mahakama ya Rufani na ndipo tukaleta upya ombi la dhamana mbele yako na Januari 17 mwaka huu, ukalisikiliza…lakini cha ajabu leo umetoa uamuzi wa kuwanyima dhamana wateja wangu wakati Jaji Mwaikugile wa mahakama hii alishatoa masharti ya dhamana …,” alidai Mapinduzi.
Alieleza kuwa sababu nyingine iliyowashangaza wateja wake na kufikia hatua ya kumkataa jaji huyo ni kwamba katika uamuzi wake huo wa maombi ya dhamana amewataja washtakiwa ni wahamiaji haramu na kwamba hawana hati za kusafiria.


MABONDIA KUPANDA ULINGONI JUMAMOS KATIKA MASHINDANO YA KLABU BINGWA


Dkt. wa Mashindano ya Taifa ya Ngumi, Joseph Magesa akimpima bondia wa Mkoa wa Ilala Jackson Mbwago kabla ya mapambano yao yanayoanza Dar es salaam lea katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa

Friday, February 25, 2011

MAPIGANO YA WAISLAMU NA WAKRISTO YAIBUKA ARUSHA

YAMEZUKA mapigano kati ya Waislam na Wakristo katika mji mdogo wa Mto wa Mbu wilayani Monduli, mkoani Arusha, na kusababisha wachungaji wawili kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Karatu kwa matibabu
Hadi tunakwenda mitamboni blogu hii ilikuwa na taarifa tofauti kuhusu chanzo cha vurugu hizo ambapo moja ilieleza kuwa chanzo cha vurugu hizo ni baadhi ya Waislamu kuwatuhumu wachungaji wawili waliotajwa kwa majina ya mchungaji Jakson na mwenzake Prospatus, kwamba wamekuwa wakiichambua vibaya Kurani tukufu hivyo kuidhalilisha dini ya Kiislam, hivyo wakaamua kuvamia mkutano wa Injili na kuwashambulia wachungaji hao pamoja na wasikilizaji wao.
Mbali na kuwajeruhi wachungaji hao, ilielezwa kuwa Waislam hao walivunja na kuliharibu kanisa la Anglikana la Mto wa Mbu.
Hata hivyo, taarifa nyingine kutoka Mto wa Mbu zilisema chanzo cha vurugu hizo ni mahubiri yaliyofanywa na mhubiri mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Utouh ambaye ilielezwa kuwa mahubiri yake aliyoyafanya kwa wiki nzima yalisababisha waumini wa Kiislam 20 wabadili dini na kuwa Wakiristo, hali ambayo ilidaiwa kuzusha chuki ya kidini katika eneo hilo.
“Walikwenda nyumbani kwa huyo mhubiri hawakumkuta, walivunja mlango wa nyumba yake na kutoa vitu vyote nje na kuvichoma moto.
“Walipotoka hapo walikwenda katika Mwalimu Anne Academy ambayo mwenye shule ni Mkiristo, hapo walivunja ofisi ya walimu ambao walikuwa madarasani na kuchukua simu za mikononi na kisha waliwapiga walimu na watoto,” zilieleza taarifa hizo kutoka kwa baadhi ya wananchi wa Mto wa Mbu waliodai kujua yaliyotokea.
 Blog hii lilipowasiliana na kamanda wa polisi, OCD Maganga, alithibitisha kupata taarifa za tukio hilo na kwamba alikuwa njiani akielekea Mto wa Mbu kulifuatilia.



MODEL OF A WEEK
 Oluchi,Nigerian super model:
Nigerian supermodel, Oluchi Onweagba-Orlandi looked stunning in the January 2011 Catalog for US Department Store, Nordstrom.
Oluchi rocked clothing from many of Nordstrom’s bestselling brands, including BCBG, Linea Pelle and DKNY.



MAPIGANO YA LIBYA YAIVA,SILAHA NZITO ZATUMIKA KUWAUA WALIBYA

Wanajeshi wanaomuunga mkono Kanali Muammar Gaddafi wametekeleza mashambulio katika miji iliyoko karibu na mji mkuu Tripoli, katika juhudi za kupanua maeneo wanayoyadhibiti.
Makabiliano makali yaliripotiwa magharibi mwa mji wa Zawiya ambapo walioshuhudia wamesema kuwa silaha nzito nzito zilitumika kuwashambulia waandamanaji ndani ya msikiti, na kuwaua takriban watu wasiopungua kumi.
Mashariki mwa mji kumetokea makabiliano makali kupigania udhibiti wa uwaja wa ndege ulioko karibu na mji wa Misurata.
Daktari mmoja ameiambia BBC kuwa hospitali yake imepokea majeruhi wapatoa 70.Mkaazi mmoja anasema wanajeshi watiifu kwa Kanali Gaddafi wamefikuzwa kutoka mji huo.
Huku hayo yakiarifiwa, rais Barack Obama wa Marekani ametoa wito kwa viongozi wa Uingereza, Ufaransa na Italia washauriane juu ya hatua za kuchukua kukabili mzozo wa Libya
Duru za awali kutoka Ikulu ya white house zilidokeza kuwa Obama anazingatia hatua kadhaa dhidi ya serikali ya Libya ikiwemo kuwekewa vikwazo.

PICHA ZA LEO:
Ben kinyaiya akiwa taabsani kwa mazoezi yanayoendelea leaders club.
Timu ya Bongo Movie Fc wameanza kujifua leo katika viwanja vya Leaders kwa ajili ya maandalizi makubwa dhidi ya Wapinzani wao Bongo Fleva Fc.Mchezo huo ambao ni maalumu kwa ajili ya kuchangia waathirika wa Mabomu ya Gongolamboto umeanza kuvuta hisia za watu na mashabiki wengi katika jiji la Dar es salaam.Kila timu inajitamba kivyake lakini sisi tunasema ushindi ni lazima siku hiyo ya jumamosi.Mashabiki mnaombwa kijitokeza kwa wingi ili kuchangia ndugu zetu wa Gongolamboto

Wizara ya sayansi na Technolojia mmeona ubunifu wa hawa watoto
Mbunifu mashuhuri Tanzania Ali rehmtulah akiwa na vazi la kipekee mmmh...!!


uniquetz t0p 40 gorgious women 2011

1. Sofia Vergara

2. Natalie Portman
 
  3. Amanda Seyfried
4. Katy Perry
5. Brooklyn Decker
6. Inez Sainz
 7. Mila Kunis

8. Selita Ebanks

9. Minka Kelly


10. Bar Rafaeli

Nawashukuru sana watu wote waliokuwa wanafatilia top 40 yetu .am magese  c u next tym.......bye bye!

Thursday, February 24, 2011

CHADEMA WAWATAJA MAFISADI JIJINI MWANZA









Mwisho wa siku wananchi haoooo...warejea makwao kwa amani na utulivu hakuna aliyeumia wala kupigwa kwenzi licha ya umati kufurika katika maandaamano na uwanjani Furahisha.
 

Chama cha maendeleo na demokrasia nchini CHADEMA leo kimefanya maandamano ya amani katika jiji la Mwanza kupinga kupinga mchakato wa uchaguzi na matokeo ya Meya wa Jiji la Arusha, kuunga mkono maandamano yaliyofanywa na chama hicho mkoani Arusha Januari 5, mwaka huu na kupinga zoezi la serikali kulipa deni la Dowans.Maelfu ya wakazi wa jiji la Miamba muda huu wamejitokeza kwa wingi kuliunga mkono zoezi hili ambalo limeanzia eneo la Buzuruga wilaya ya nyamagana na kuelekea katika viwanja vya Furahisha wilayani Ilemela ambapo kutakuwa na mkutano.

MabangozZZZ!!..

Hali ya hewa barabara ya Kenyeta.

Mmiliki wa dowans aka.....

Barabara ya Makongoro kuelekea kata ya Kirumba uwanja wa Furahisha eneo ambako mkutano utafanyika jioni ya leo.

Ujumbe kwa wakazi wa Gongo la mboto toka CHADEMA Mwanza.

Pikipiki eneo la kipita shoto cha ilipokuwa sanamu ya baba wa taifa.
(PICHA NA;gsengo) 

 MUSTAFAH KUJA NA MPYA
Mustafa Hassanali addresses a safe motherhood campaign during press conference held at Habari Maelezo today, right is Ms Rose Mlay, the country coordinator of White Ribbon Alliance and Safe Motherhood in Tanzania.
Yale maonyesho ya mavazi yajulikanayo kama ‘mamma mia’ yenye nia ya kuhamasisha uzazi salama, sambamba na sherehe za miaka 50 ya uhuru Tanzania, na miaka mia moja ya siku ya mwanamke duniani , kwa kushirikiana na shiriki lisilo la kiserikali la utepe mweupe ‘White Ribbon Alliance’ na ‘Vodacom Foundation’, yazinduliwa rasmi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, mbunifu wa mavazi, aliyejipatia umaarufu kitaifa na kimataifa, Mustafa Hassanali amesema “ntazindua toleo langu jipya la ki-afrika katika maonyesho haya ya ‘Mamma Mia’ siku ya tarehe 4 na tano mwezi Machi hapahapa jijini Dar es salaam, na nategemea kupata ushirikiano wa watu wote, katika kuhamasisha uzazi salama kwa msaada wa shirika la utepe mweupe”

‘Mamma Mia’ ni jukwaa la  maonyesho ya mavazi ambalo limelengwa mahsusi katika kusambaza ujumbe kuhusu uzazi salama, litafanyika tarehe nne mwezi machi, katika hoteli ya ‘Moevenpick Royal Palm’ kuanzia saa mbili na nusu usiku, na onyesho jingine kwa siku ya Jumamosi ya tarehe tano  kuanzia saa tisa na nusu jioni, katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

MREMBO WA WIKI

Susana Luiz

Mapigano makali yazuka Somalia


Somalia
Mapigano makali yanaarifiwa kutokea katika maeneo matatu nchini Somalia.
Mwaandishi wa BBC anasema haya ni mapigano makali kabisa kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa kundi la wanaharakati wa kiislamu la Al-Shabab, katika mji mkuu, Mogadishu, katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
Vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika, inasemekana vimeiteka ngome kuu ya al-Shabaab .
Kuna taarifa za kutokea mapambano katika mji wa Beledweyne kwenye mpaka wa Ethiopia na Bulahawa, na kwenye mpaka na Kenya.
Mapigano makali ya mjini Mogadishu yaliendelea siku nzima Jumatano.
Wanajeshi kutoka Burundi ambao ni sehemu ya jeshi la Muungano wa Afrika wamekuwa wakipigana bega kwa bega na wanajeshi wa serikali hiyo ya mpito ya Somalia.
Wamefanikiwa kuyateka maeneo ya wapiganaji wa Al Shabab baada ya kusonga mbele mtaa kwa mtaa.
Eneo liliotekwa ikiwemo iliyokuwa wizara ya ulinzi ni dogo lakini ni muhimu katika mikakati ya kijeshi.
Kundi la Al Shabab pia limekabiliwa na shinikizo katika mji wa Beledweyne kwenye mkoa wa kati wa Somalia ambako wanajeshi wa serikali na wanamgambo washirika wamekuwa wakifanya mashambulizi.
Katika medani ya tatu ya mapigano Bula Hawo karibu na mpaka wa Kenya wapiganaji wanaohusishwa na kundi la Al Qaeda walishambuliwa na kundi jingine la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.
Ingawa mpaka huo umefungwa rasmi , wakazi wamekuwa wakikimbia mapigano ya huko na kuelekea mji wa Mandera nchini Kenya.

Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alihutubia waandishi wa habari mjini Mogadishu.
Akiwa amevalia sare ya kijeshi , aliwasifu wanajeshi wa serikali na kusisitiza kwamba mashambulio hayo katika maeneo tofauti yameratibiwa.
Jeshi la Muungano wa Afrika na wanajeshi wa serikali wanazungumzia kuendelea kulivunja nguvu kundi la Al Shabab, hata hivyo kundi hili la msimamo mkali wa kiislamu bado linadhibiti maeneo makubwa ya nchi na linaweza kusababisha vurugu kubwa.
Siku ya Jumatatu bomu liliotegwa ndani ya gari liliwaua watu wasiopungua 17 karibu na kituo cha mafunzo ya polisi mjini Mogadishu.


SHEKH YAHYA ATABIRI SERIKARI YA JK KUYUMBA

 SHEIKH YAHYA HUSSEIN

 Mnajimu maarufu nchini Tanzania yahya hussein ametoa utabiri wake leo jijini Dar kuwa wizara ya Elimu,Bodi ya mikopo zitayumba ikiandamwa na kashfa pamoja maandamano na migomo kadhaa kuwepo kwa mwaka huu


WAKAZI WA KOTA ZA BANDARI WAFANYA MKUTANO WA KUMPINGA MKUCHIKA

Mwanasheria wa Kampuni ya Kibasila Estates Public Limited. Dkt. Sengondo Mvungi akifafanua jambo wakati wa mkutano wa dharula na wateja wake Kota za Bandari Dar es Salaam baada ya taarifa ya Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw.George Mkuchika kusikika akisema kupitia vyombo vya habari kuwa watu hao wamelipwa na wanatakiwa kobomoa nyumba zao ambapo kesi yao ya msingi haijatajwa na na hawajalipwa