
Aliyekuwa Rais wa Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali  anaumwa sana na amelazwa katika hospitali ya Saudi Arabia. 
Mtu wa karibu wa familia yake ameliambia shirika  la habari la AFP, Bw Ben Ali, aliyeondolewa wakati wa ghasia  zilizoibuka mwezi uliopita, amepata kiharusi.
Bw Ali mwenye umri wa miaka 74 alikimbilia Saudi  Arabia na familia yake baada ya kuwepo maandamano makubwa kwa wiki  kadhaa juu ya ukosefu wa ajira na umaskini.
Tunisia kwa sasa ina serikali ya mpito  inayoiandaa nchi kwa uchaguzi mkuu.
Jamaa huyo, ambaye jina lake halikutajwa,  alisema aliyekuwa Rais yupo "kwenye hali ya kuzimia" katika hospitali  moja mjini Jeddah.
Alisema, "alipata kiharusi , na hali yake ni  mbaya sana."
Gazeti la Tunisia liitwalo Le Quotidien pia  liliripoti siku ya Alhamis kwamba Bw Ben Ali amepata kiharusi.
Wakati huo huo, chanzo cha Saudi Arabia  kilichonukuliwa na shirika la habari la Reuters limesema Bw Ben Ali  alikuwa "katika hali mbaya."
Awali, msemaji wa serikali ya mpito ya Tunisia  amekataa kuthibitisha au kukubali taarifa zozote kuwa Ben Ali yuko  hospitali. VODACOM YATOA MSAADA KWA WAHANGA WA MABOMU
Mkurugenzi  wa mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akiwa amebeba  kapu  lenye mikate kwa ajili ya waadhirika wa janga la ulipukaji wa mabomu  Gongo la mboto waliopo katika kiwanja cha uhuru,Vodacom Foundation  ilitoa misaada mbalimbali .
  LAMPARD AIONYA CHELSEAFrank Lampard amekiri itakuwa  "maafa" iwapo Chelsea itashindwa kufuzu Ligi ya Ubingwa wa Ulaya msimu  ujao.
Frank  Lampard
Sare ya kutofungana dhidi ya Fulham siku ya  Jumatatu, imewafanya mabingwa hao watetezi kusalia nafasi ya tano ya  msimamo Ligi Kuu ya soka ya England.
Chelsea kwa sasa wapo nyuma kwa pointi 12 ya  vinara wa ligi hiyo, Manchester United.
Akizungumza katika uzinduzi wa Wakfu wa Wacheza  Soka wa England, Lampard ameiambia BBC kitengo cha michezo : "Hatuna  budi kumaliza katika timu nne za juu na kamwe hatupaswi kupoteza michezo  zaidi, itakuwa "maafa" iwapo hatutafaulu."
Chelsea siku ya Jumamosi itakabiliana na Everton  katika mzunguko wa nne wa hekaheka za kuwania Kombe la FA na  watapepetana na FC Copenhagen katika mchezo wa kwanza wa mtoano wa Ligi  ya Ubingwa wa Ulaya siku tatu baadae.
Na Lampard amekiri mashindano hayo mawili ni  muhimu sana kwa klabu yao.
Msambuliaji aliyesajiliwa kwa kitita cha paundi  milioni 50 na Chelsea, Fernando Torres ameshindwa kufunga katika mechi  mbili alizocheza. Torres alinyakuliwa kwa kitita hicho kutoka Liverpool,  lakini Lampard amemtetea nyota huyo wa Hispania katika klabu yake mpya.
Kuhusu mlinzi Luiz aliyesajiliwa kwa paundi  milioni 25, Lampard amesema amefurahishwa na usajili walioufanya katika  dirisha dogo la usajili mwezi wa Januari, ambapo klabu hiyo imetumia  paundi milioni 75.
MTOKO WA JUSTINE BIEBER TOKA KWA D&G
WE caught up with Stefano Gabbana and Domenico Dolce this morning, as  they prepare for their Milan show, to see how the designers feel about  being the label of choice for the most Googled person on the planet:  Justin Bieber. The 16-year-old singer wore a D&G waist coat, bow  tie, shirt and jeans as he arrived at the O2 Arena for the premiere his  biopic, Never Say Never, where hoards of screaming tweens took  part in scenes of mania not seen since the days of The Beatles.
"Justin represents the epitome of the new generation of music  talents," Stefano Gabbana told us. "We are fascinated by his capability  of communicating with his music to a wide variety of audiences, from the  teenagers to a more adult public."
 
 

No comments:
Post a Comment