
(PICHA NA;gsengo) 
 MUSTAFAH KUJA NA MPYA
Mustafa  Hassanali addresses a safe motherhood campaign during press conference  held at Habari Maelezo today, right is Ms Rose Mlay, the country  coordinator of White Ribbon Alliance and Safe Motherhood in Tanzania.
Yale  maonyesho ya mavazi yajulikanayo kama ‘mamma  mia’ yenye nia ya  kuhamasisha uzazi salama, sambamba na sherehe za miaka 50 ya  uhuru  Tanzania, na miaka mia moja ya siku  ya mwanamke duniani , kwa  kushirikiana na shiriki lisilo la kiserikali la utepe  mweupe ‘White  Ribbon Alliance’ na ‘Vodacom Foundation’, yazinduliwa  rasmi.
Akizungumza  katika uzinduzi huo, mbunifu wa mavazi,  aliyejipatia umaarufu kitaifa  na kimataifa, Mustafa Hassanali amesema “ntazindua  toleo langu jipya la  ki-afrika katika maonyesho haya ya ‘Mamma Mia’ siku ya  tarehe 4 na  tano mwezi Machi hapahapa jijini Dar es salaam, na nategemea kupata   ushirikiano wa watu wote, katika kuhamasisha uzazi salama kwa msaada wa  shirika  la utepe mweupe”
‘Mamma Mia’ ni jukwaa la  maonyesho  ya mavazi ambalo limelengwa  mahsusi katika kusambaza ujumbe kuhusu  uzazi salama, litafanyika tarehe nne  mwezi machi, katika hoteli ya  ‘Moevenpick Royal Palm’ kuanzia saa mbili na nusu  usiku, na onyesho  jingine kwa siku ya Jumamosi ya tarehe tano  kuanzia saa tisa na nusu jioni, katika  viwanja vya Mnazi Mmoja.
Somalia
Mapigano makali yanaarifiwa kutokea katika maeneo matatu nchini Somalia. 
Mwaandishi wa BBC anasema haya ni mapigano  makali kabisa kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa kundi la  wanaharakati wa kiislamu la Al-Shabab, katika mji mkuu, Mogadishu,  katika kipindi cha miezi michache iliyopita.Vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika, inasemekana vimeiteka ngome kuu ya al-Shabaab .
Kuna taarifa za kutokea mapambano katika mji wa Beledweyne kwenye mpaka wa Ethiopia na Bulahawa, na kwenye mpaka na Kenya.
Mapigano makali ya mjini Mogadishu yaliendelea siku nzima Jumatano.
Wanajeshi kutoka Burundi ambao ni sehemu ya jeshi la Muungano wa Afrika wamekuwa wakipigana bega kwa bega na wanajeshi wa serikali hiyo ya mpito ya Somalia.
Wamefanikiwa kuyateka maeneo ya wapiganaji wa Al Shabab baada ya kusonga mbele mtaa kwa mtaa.
Eneo liliotekwa ikiwemo iliyokuwa wizara ya ulinzi ni dogo lakini ni muhimu katika mikakati ya kijeshi.
Kundi la Al Shabab pia limekabiliwa na shinikizo katika mji wa Beledweyne kwenye mkoa wa kati wa Somalia ambako wanajeshi wa serikali na wanamgambo washirika wamekuwa wakifanya mashambulizi.
Katika medani ya tatu ya mapigano Bula Hawo karibu na mpaka wa Kenya wapiganaji wanaohusishwa na kundi la Al Qaeda walishambuliwa na kundi jingine la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.
Ingawa mpaka huo umefungwa rasmi , wakazi wamekuwa wakikimbia mapigano ya huko na kuelekea mji wa Mandera nchini Kenya.
Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alihutubia waandishi wa habari mjini Mogadishu.
Akiwa amevalia sare ya kijeshi , aliwasifu wanajeshi wa serikali na kusisitiza kwamba mashambulio hayo katika maeneo tofauti yameratibiwa.
Jeshi la Muungano wa Afrika na wanajeshi wa serikali wanazungumzia kuendelea kulivunja nguvu kundi la Al Shabab, hata hivyo kundi hili la msimamo mkali wa kiislamu bado linadhibiti maeneo makubwa ya nchi na linaweza kusababisha vurugu kubwa.
Siku ya Jumatatu bomu liliotegwa ndani ya gari liliwaua watu wasiopungua 17 karibu na kituo cha mafunzo ya polisi mjini Mogadishu.
SHEKH YAHYA ATABIRI SERIKARI YA JK KUYUMBA
 
 


No comments:
Post a Comment