Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Saturday, February 26, 2011

SHILOLE ATANGAZA VITA NA WALA VIRINGI

Msanii chipukizi wa filamu Zena mohamed "shilole" amethubutu kudai kwa kukieleza moja vyombo vya habari kuwa hashobokei mapapaa"wala viringi".
Licha ya binti huyo kuwa na shepu ya kuwastua wanaume wengi wenye fedha zao hapa mjini shilole kadai sio limbukeni wa kushobokea mafweza ana true love kwa muhusika wake.
Hebu tufuatilie kwa kina kama miezi kadhaa atadumisha hiyo kauli yake kwani kujigamba huko kumewakwaza sana wakwale hao.

 UN yamwekea vikwazo Gaddafi
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura - na kupita bila kupingwa - ya kuuwekea vikwazo utawala wa Muammar Gaddafi kutokana na hatua yake ya kutaka kuzima maandamano.
UN
Wajumbe wa UN wakipiga kura ya vikwazo kwa Gaddafi
Baraza hilo limeunga mkono kuweka vikwazo vya silaha na kupiga tanji amana, huku wakifikisha suala hilo katika Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinaadamu.
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kiongozi huyo wa Libya aondoke madarakani na kuondoka nchini humo.
Hata hivyo bado anadhibiti mji wa Tripoli, lakini upande wa mashariki wa nchi unashikiliwa na waadamanaji.
Majadiliano ya kuunda serikali ya mpito ya wanaompinga Gaddafi inaarifiwa yanafanyika.
Mustafa Abdel-Jalil, aliyejiuzulu uwaziri wa sheria kwa kupinga matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji amesema tume yenye raia na wanajeshi itaandaa uchaguzi katika kipindi cha miezi mitatu, limekaririwa gazeti binafsi Quryna.
Libya
Waandamanaji Benghazi
Mabalozi wa Libya nchini Marekani na katika Umoja wa Mataifa wameunga mkono mpango huo, ambao unajadiliwa katika mji wa mashariki unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi.
Umoja wa Mataifa (UN) unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wamekufa, wakati utawala wa Kanali Gaddafi ukijitahidi kuzima vuguvugu la mabadiliko lililodumu kwa siku kumi.
Hii ni mara ya pili tu kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufikisha nchi katika ICC, na ni kwa mara ya kwanza kura kama hiyo kupita bila kupingwa.


 WANAJESHI WATOA KICHAPO GONGO LA MBOTO
    kichapo hiko kilitolewa na wanajrshi mida ya sita usiku kwa kuwadunda raia kwa mabuti,makofi na virungu,imeripotiw a watu 8 kujerhiwa na mkong"oto huo madhubuti.

    Yapata takriban tisa baada ya Dar es Salaam kutikiswa na milipuko ya mabomu na makombora katika kikosi cha Jeshi cha 511 ambacho ni Ghala Kuu la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Gongo la Mboto, askari zaidi ya 30 wa kikosi hicho wanadaiwa kupiga raia.
Askari hao inadaiwa waliwapiga raia hao usiku wa kuamkia jana kwa madai ya kulipiza kisasi baada ya mwenzao kupigwa na raia wa eneo hilo.
 WALIBYA WAJIAMDAA KWA VITA DHIDI YA GADDAFI
Watu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli wanajiandaa kwa mapambano zaidi, baada ya kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi kusema atafungua maghala ya silaha kwa ajili ya wanaomuunga mkono.
Gaddafi
Kanali Gaddafi
Uondoaji wa maelfu ya wafanyakazi wa kigeni unaendelea kwa njia ya anga, bahari na barabara, lakini wengine bado wamekwama.
Marekani imezuia matumizi yoyote ya fedha na amana za Kanali Gaddafi na baadhi ya watu wake wa karibu.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wamekufa katika mzozo wa kisiasa wa siku 10.
Siku ya Ijumaa, waandamanaji wanaopinga serikali mjini Tripoli wameshambuliwa kwa nguvu na bunduki.
Shirika la habari la AP limesema, limeelezwa kuwa serikali ya Kanali Gaddafi inawapa silaha raia wanaoiunga mkono ili kuweka vizuizi mjini Tripoli na kuwabana waandamanaji.
Wakazi ambao wamezungumza na AP kwa njia ya simu siku ya Jumamosi, wameripoti kuwa magari ya raia wanaomuunga mkono Kanali Gaddafi yanafanya doria mitaani.


BONGO FLAVA FC YAILAMBA BONGO MOVIE FC 2-0 

   Kikosi cha Bongo flava fc
Kikosi cha Bongo MOVIE FC

Meya wa Manispaa ya Ilala Jelly Slaa akisalimiana na 'Muuaji' wa Bongo Movie H.Baba.
 

WASHIRIKI WA MISS UTALII WANGOJEA SIKU

Jumla ya warembo 45 wanaotaraji kushiriki katika kinyang'anyiro cha kumsaka miss utalii Tanzania mwishoni mwa wiki ijayo tarehe 5 march 2011,wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Dar es salaam baada ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari na Rais wa Miss Utalii Tanzania Gideon Chipungahelo. Mshindi wa shindano hilo anataraji kuondoka na mkataba wenye thamani ya shilingi milioni 150 ambao utajumuisha kusomeshwa chuo kikuu, gari, fedha za kujikimu na naulishindano hilo litafanyika wilayani Bagamoyo jumamosi ijayo.MISS TZ AENDA CHINA LEO
Mrembo mwenye mvuto na mshindi wa taji la Miss Tanzania 2010/2011Geneviev Emanuel  ameondokas leo kwa ndege kuelekea china kwa takribani wiki tatu.

TUNISIA WAANZA MAANDAMANO UPYA Polisi wamewatawanya waandamanaji katika mji mkuu wa Tunis siku ya Ijumaa wakidai kujiuzulu kwa Mohammed Ghannouchi, ambaye amekuwa akiongoza nchi hiyo baada ya Ben Ali kuikimbia Tunisia mapema mwaka huu.

Waandamanaji nchini Tunisia
Waandamanaji nchini Tunisia
Ulikuwa umati mkubwa zaidi tangu Rais Ben Ali kuikimbilia Saudi Arabia mwezi uliopita.
Ben Ali alikuwa Rais wa Tunisia kwa kipindi cha miaka 23 na alitimuliwa baada ya wiki kadhaa za maandamano.
Bw Ghannouchi na serikali yake ya mpito walitangaza wataanda uchaguzi utaofanyika mwezi wa Julai.
Lakini waandamanaji wanaonekana kutoridhishwa na walikuwa wakiimba mitaani 'Ghannouchi ondoka.'
Polisi walifyatua risasi za ilani na mabomu ya kutoa machozi karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Walioshuduia tukio hilo wanasema mtu mmoja tu ndiye aliyejeruhiwa miongoni mwa waandamanaji takriban 100,000.
Bw Ghannouchi aliwahi kufanya kazi katika serikali ya Ben Ali tangu mwaka 1999.


PICHA ILIOMTIA RIHANNA MATATANI 

Mwili wa Rihaana ilipigwa na chriss beez enzi za uhai wa penzi lao


 KESI YA MAGUFULI WASHTAKIWA WAGOMA
John MagufuliHATIMAYE raia 34 wa kigeni wanaokabiliwa na kesi ya uvuvi haramu kwenye ukanda wa Bahari ya Hindi maarufu “Kesi ya Samaki wa Magufuli’ jana waligeuka mbogo na kumuomba Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Radhia Sheikh, ajitoe kusikiliza kesi hiyo kwa sababu hawana imani naye.
Ombi hilo liliwasilishwa na mawakili wa washtakiwa hao, John Mapinduzi na Ibrahimu Bendera, mahakamani hapo ikiwa ni saa chache baada ya jaji huyo kutoa uamuzi wa kuwanyima dhamana licha ya kifungu cha 148 (6) na (7) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, makosa yanayowakabili washtakiwa kuwa na dhamana.
Sababu ya jaji huyo kuwanyima dhamana ni kwamba mazingira ya kesi hiyo washtakiwa wakipewa dhamana wanaweza wakaruka.
“Wateja wangu wamenieleza kuwa hawana kabisa imani na wewe na wanaomba ujitoe uongozi wa mahakama umpange jaji mwingine kwa sababu wanaamini dhamana ni haki yao.
“Wateja wangu wamenieleza kwamba kilichowashtua zaidi ni kwamba mapema mwaka jana jaji wa mahakama hii, Njegafibili Mwaikugile, alishatoa masharti ya dhamana kwa wateja wangu na ambapo wateja wangu walikimbilia Mahakama ya Rufani na jopo la majaji wa rufani watatu waliokuwa wakiongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Agustino Ramadhan liliamuru ombi hilo la washtakiwa la kutaka wapatiwe waliwasilishe Mahakama Kuu na mahakama hiyo isikilize ombi hilo.
“Mimi pamoja na wateja wangu tulitekeleza amri ya Mahakama ya Rufani na ndipo tukaleta upya ombi la dhamana mbele yako na Januari 17 mwaka huu, ukalisikiliza…lakini cha ajabu leo umetoa uamuzi wa kuwanyima dhamana wateja wangu wakati Jaji Mwaikugile wa mahakama hii alishatoa masharti ya dhamana …,” alidai Mapinduzi.
Alieleza kuwa sababu nyingine iliyowashangaza wateja wake na kufikia hatua ya kumkataa jaji huyo ni kwamba katika uamuzi wake huo wa maombi ya dhamana amewataja washtakiwa ni wahamiaji haramu na kwamba hawana hati za kusafiria.


MABONDIA KUPANDA ULINGONI JUMAMOS KATIKA MASHINDANO YA KLABU BINGWA


Dkt. wa Mashindano ya Taifa ya Ngumi, Joseph Magesa akimpima bondia wa Mkoa wa Ilala Jackson Mbwago kabla ya mapambano yao yanayoanza Dar es salaam lea katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa

No comments: