Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, February 23, 2011

WAZIRI WA MICHEZO ANAEPENDA TOTOOZI ILE MBAYA!!

               Bata mwanzo mwisho mtu wangu ....ponda mali kufa kwaja!!

waziri Joseph Habineza wa Rwanda akiwa na totoozi enzi za miaka ya 2008 akiyachapa maisha huku akipata kilevi vya kutosha katika nyumba moja huko kigari,picha zilizowekwa na mwanafunzi mmoja wa huko Rwanda akimuonyesha waziri Hebeneza akiponda raha kitu ambacho kilimpelekea kujiuzulu madaraka yake hivi karibuni

 

 FFU vs CHADEMA 

KWA mara nyingine tena Jeshi la Polisi jana lilitumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wakimsindikiza ofisini mbunge wao, Godbless Lema, mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya kufanya kusanyiko kinyume cha sheria inayomkabili pamoja na viongozi wakuu wa chama hicho.

Katika hali isiyo ya kawaida Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) na wafuasi hao walionekana wakigombea maganda ya risasi na mabomu yaliyokuwa kwenye eneo hilo ambapo polisi walikuwa wakiwakimbiza wananchi walioyachukua na kuwanyang’anya huku wengine wakifanikiwa kutokomea nayo.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa nne asubuhi wakati wananchi hao na Lema walipokuwa wamefika mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakielekea jengo la Mkuu wa Wilaya ya Arusha zilipo ofisi za mbunge huyo, hata hivyo hakukuwa na taarifa zozote za watu kujeruhiwa.
Askari hao wawili waliokuwa kwenye magari mawili akiwemo mkuu wa polisi wa wilayani hapa (OCD), Zuberi Mwombeji, aliyekuwa kwenye gari lenye namba za usajili PT 1844 walilipita kundi hilo la watu na kwenda mbele kidogo kisha polisi walishuka kwenye magari yao na kuanza kufyatua mabomu ya machozi na kupiga risasi za moto hewani ambapo baadhi ya wananchi walitawanyika huku wengine wakiendelea kutembea na mbunge wao mpaka walipohakikisha wameingia ndani ya uzio wa ofisi za mkuu wa wilaya.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, Akili Mpwapwa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukiri kuwa walitumia mabomu kuwatawanya wafuasi hao wa CHADEMA kwa sababu ya kile alichodai kuwa walikuwa wakiimba salamu yao ya “People’s Power – Nguvu ya Umma” ambayo iliwavutia watu wengi na kujiunga kwa wingi katika matembezi hayo ya kumsindikiza mbunge huyo ofisini kwake.


   UNCLE SULEIMAN AL ADAWI AJIWEKA HADHARANI

MNYONGE Mtanzania na zigo la Dowans kwa Tanesco katika mtazano wa Katuni.

Miliki wa Dowans, Suleiman Al Adawi ameibua mjadala mzito nchini tangu alipotua na kufanya mkutano na wahariri wa magazeti matano Jumapili iliyopita, akigoma kupigwa picha pia akizuia televisheni na redio, huku akificha sura yake na sauti. Hata hivyo, mbio hizo za Al Adawi kukwepa kamera za waandishi jana ziliishia ukingoni baada ya kunaswa na kamera za gazeti la Mwananchi wakati akikagua mali zake zilizopo Ubungo.

Mpango mkakati wa kumnasa Al Adawi, ulipangwa na kufanikishwa kwa pamoja na duru huru za habari kutoka kwa raia wema ambao, awali walidokeza kuwa bosi huyo wa Dowans angefanya ziara kukagua mitambo ya kampuni hiyo mapema asubuhi. Swali ni kwamba nini kitafuata baada ya hili....

 

 30 Best Ever Oscar Dresses


Feida pinto.

The nominations are out and the tuxedos and gowns are being picked – it’s time for the 83rd Annual Academy Award

While predictions are doing the rounds about who the gold man will belong to this year, we are more concerned about which couture gown will the starlets walk the red carpet in.

From Million Dollar Baby, Hillary Swank in a Guy Laroche to Carey Mulligan’s quirky Prada dress, the red carpet leading to the Kodak Theatre that can make or break an actor’s style potentials.

With the upcoming Oscars we take a look at the best dresses to grace the red carpet

.

 WANAJESHI WA GDAGBO WAUWAWA IVORY COASTY

Wanajeshi wa Ivory Coast
Wanajeshi wasiopungua 10 watiifu kwa kingozi aliyekatalia madarakani nchini Ivory Coast, Laurent Gbagbo, wanaripotiwa kuuwawa katika vurungu katika mji mkuu wa nchi hiyo Abidjan.
Ripoti kutoka nchini humo zinasema, wanajeshi wa Bw Laurent Gbagbo walishambulia eneo linalo muunga mkono kiongozi anayetambulika na jamii ya kimataifa kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa mwaka uliopita, Alassane Ouattara.
Walioshuhudia wanasema wanajeshi watiifu kwa rais Gbagbo waliwapiga risasi wafuasi wa Bw Ouattara, na kuwauwa watu sita.
Vifo hivyo vinatokea huku jaribio la hivi karibuni la viongozi wanne wa Afrika likiendelea kujaribu kutafuta suluhu la mzozo nchini Ivory Coast.


KANUMBA: TUSILAUMIWE KUPOROMOKA KWA MAADILI

Muigizaji wa filamu nchini,Steven Charles Kanumba (Katikati) akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa kuhusu Harakati za kuivusha tasnia ya filamu katika ngazi za kimataifa.Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego na Mratibu wa jukwaa hilo,Ruyembe C.Mulimba.
Mratibu wa Jukwa la Sanaa,Bw.Ruyembe akisisitiza jambo juu ya harakati za kuivusha tasnia ya filamu kwenye ngazi ya kimataifa.Katikati ni muigizaji Kanumba na Katibu Mtendfaji wa BASATA,Materego.

Libya: Gaddafi agoma kung"atukaka!!

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amegoma kuondoka madarakani licha ya kuwepo kwa maandamano makubwa ya kupinga serikali, ambayo amesema yamechafua sura ya nchi.
gaddafi
Muammar Gaddafi
Katika hotuba yake kubwa tangu kuanza kwa vuguvugu wiki iliyopita, Kanali Gaddafi amesema dunia nzima inaitazama Libya na kuwa maandamano hayo yana "mhudumia shetani".
Akisoma vifungu kutoka ndani ya katiba ya nchi hiyo, amesema maadui wa Libya watauawa.
Makundi ya haki za binaadam yanasema karibu watu 300 wameuawa hadi sasa katika ghasia.


VIBWEKA VYA MASTAA 
Mtu mzima shaq akidendeka
 Kanye west akidendeka na Amber rose
jamaani njoo tuogelee............mi staki na sikia baridi mwezio



No comments: