Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, February 16, 2011


BONDIA wa Zamani na Kocha wa Ngumi wa Klabu ya ngumi ya Ashanti, Rajabu Mhamila 'Super D' yupo mbioni kutoa Video inayozungumzia maisha yake ya mchezo huo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Super D alisema video hiyo itakuwa sokoni muda wowote kuanzia sasa ikizungumzia maisha yake tangu alipoanza kucheza mchezo huo mwaka 1984 hadi 2010 sasa.

Alisema Video hiyo itaonesha mapambano mbalimbali aliyocheza na dhidi ya mabondia Mbwana Matumla, Rashidi Ali na Ajibu Salumu.

Alisema lengo la kuandaa video ni kutaka kutimiza malengo yake ya kuendeleza mchezo wa ngumi kwa kuwapatia vijana nafasi ya kujifunza kupitia kwake.

Alisema kutokana na nchi ya Tanzania kuwana vipaji vingi atashindwa kuwafikia kila mmoja wao na badala yake amewapa fursa ya kujifunza kwa kuangalia video.

Alisema Video katika kuhaikisha Video hiyo inafanya vizuri sokoni ameongezea vionjo vingine kutoka kwa mabondia maarufu duniani kama Mike Tyson, Michael Mo,Junior Myweather, Mohamed Ally, Man Paqyao na Joe Fleizer.
 

No comments: