Naibu Spika wa Bunge la Tanzania
Fredy Azzah
NAIBU
Spika wa Bunge, Job Ndugai amemjia juu Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick
Sumaye kuhusu kauli yake ya posho za wabunge, akisema hakupaswa kuitoa
kwani aliwahi kufanikisha kupitishwa sheria ya malipo kwa viongozi wakuu
wastaafu ili kujinufaisha akistaafu.Juzi, Sumaye pamoja na mambo
mengine, alizungumzia mwelekeo wa taifa kwa sasa na kuelekea Uchaguzi
Mkuu wa 2015 huku akisema mpango wa ongezeko la posho za wabunge
unapaswa kuachwa kwani unaweza kufanya makundi mengine ya utumishi wa
umma kudai nyongeza.
Kauli
hiyo ilijibiwa vikali jana na Ndugai ambaye aliwatahadharisha viongozi
wastaafu kuwa makini na kauli wanazotoa na kuwataka wale ambao wanataka
urais wa 2015 ikiwa ni pamoja na Sumaye waseme sasa badala ya
kuwababaisha Watanzania kwa kuzungumza mambo mbalimbali ili wawapende.
Alisema
wakati Sumaye anazungumzia posho za wabunge, sheria ya kuwalipa
viongozi wastaafu mafao ilipitishwa wakati akiwa kiongozi wa shughuli za
Serikali bungeni na hakuipinga kwa kuwa alikuwa anajiandalia mazingira
ya kustaafu.
“Kwa
sasa analipwa asilimia 80 ya mshahara wa waziri mkuu aliyepo
madarakani, ni fedha nyingi kuliko hata mshahara wa Naibu Spika (Ndugai
kwa sasa), wakati sheria hii inapitishwa alikuwa kiongozi wa shughuli za
Serikali bungeni (Waziri Mkuu), alikuwa anajiandalia mazingira ya
kustaafu,” alisema Ndugai na kuongeza:
“Sitaki
kuendelea kusema sana jinsi ambavyo ananufaika, lakini ninachosema
viongozi wastaafu duniani kote inatakiwa wawe makini na kauli zao.
Wakianza kwenda kwenye vyombo vya habari na kusema maneno haya
haipendezi.”
Alifafanua
kwamba badala ya kuzungumzia posho za wabunge pekee ni vyema pia
likazungumziwa suala la posho kwa viongozi wote wa umma.
No comments:
Post a Comment