MSHINDI
wa pili wa ligi kuu ya Zanzibar timu ya Jamhuri yenye mastakimu yake
mtaa wa chasasa kisiwani Pemba jana waliianza vyema michuano ya
mapinduzi Cup baada ya kuifunga timu ya Simba ya Dar es salaam mabao 2-1
katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wawanja Amani mjini Zanzibar
Mechi
hiyo kati ya Simba na Jamhuri ambayo ilichezeshwa na mwamuzi Juma Ali
ilikuwa ya kuvutia na ya kupendeza hadi kipindi cha kwanza kinamalizika
hakuna timu ambayo ililiona lango la mwenzake japo kuwa juhudi za
kufunga zilikuwa zimefanyika kwa timu zote lakini kwa bahati mbaya
hakuna timu ilifunga kipindi hicho cha kwanza.
Katika
mechi hiyo ambayo ilihudhuriwa na wapenzi wengi wa soka wa Zanzibar
ilikuwa ni timu ya Jamhuri ambayo ilipata bao la kwanza lililofungwa na
mshambuliaji Ali Othman Mmanga katika dakika ya 10 ya kipindi cha pili
cha mchezo huo
Kama
hiyo haitoshi timu ya Jamhuri ambayo ilikuwa ikicheza kwa uwelewano
mkubwa iliandika bao la pili katika dakika ya 21 bao hilo lilifungwa na
Ali Bakar na kumuacha mlinda mlango wa Simba Ali Mustafa Batezi akiwa
hana la kufanya
Timu
ya Simba itashiriki katika michuano ya kombe la shirikisho na ambayo
ilikuwa imechezesha wachezaji mchanganyiko wale wa zamani na damu changa
kutokana na uzoefu wao kabla ya kumalizika kwa pambano hilo walipata
bao la kufutia machozi bao ambalo lilifungwa na beki wao anayepanda na
kushuka Shomari Kapombe
Kocha
wa timu hiyo ya Simba alipoulizwa juu ya pambano hilo kwanini amepoteza
mchezo huo alisema kuwa mabeki wa timu, hiyo walifanya makosa ambapo
wenzao wa timu ya Jamhuri wameyatumia na kushuinda mchezo huo
Kabla
ya kufungwa kwa timu ya simba hapo jana mabao 2-1 katika mfululizo wa
michuano ya kombe la Mapinduzi Cup, timu ya Yanga nayo ya Dar es salaam
tayari imekwisha fungwa bao 1-0 na timu ya Mafunzo ya Zanzibar
Katika
kinyanganyiro hiki cha michuano ya kombe la Mapinduzi kutimia miaka 48
timu zinazoshiriki katika michuano hiyo ni pamoja na timu ya Jamhuri,
Mafunzo, Kikwajuni, Yanga, Simba, na timu ya Azam FC wanaramba ramba
Aidha
katika mashindano hayo ya mapinduzi Cup kutimiza miaka 48 ya mapinduzi
ya Zanzibar pia zipo timu za kikosi maalumu cha kuzuia magendo KMKM
pamoja na Miembeni United.
No comments:
Post a Comment