BREAKING NEWS: ANASWA NA UMEME AKIIBA MAFUTA YA TRANSFOMA
Mtu
mmoja ambaye hajatambulika jina lake amenaswa na umeme wa transfoma
usiku wa kuamkia leo katika eneo la Hospitali ya Bugando jijini Mwanza
na kufariki dunia papo hapo. Taarifa za uchunguzi zinamtaja mtu
huyo ambaye inasemekana kuwa alikuwa katika mchakato wa kuiba mafuta ya
transfoma hilo, wakati akifanya wizi huo alinasa mara baada ya kuegemea
bila kujua moja ya nyaya zilizokuwa na umeme. Mafundi wa umeme kutoka Tanesco wakipanda kuunasua mwili wa jamaa huyo. Kutokana
wizi huo baadhi ya maeneo ya jiji la Mwanza hususani eneo la Hospitali
ya Bugando na maeneo yake ya jirani yamekosa umeme usiku mzima hadi leo
na baadhi ya shughuli kusimama kwa kukosa nishati ya umeme. Asubuhi
ya leo mashuhuda kutoka sehemu mbalimbali walimiminika kwenye tukio
hilo la kutisha na kuona hatua kwa hatua za ushushaji wa mwili wa mwizi
huyo wa mafuta ya transfoma. TANESCO
kupitia kitengo chake cha usalama, kimekuwa kikifuatilia kwa ukaribu
hali hiyo, ili kupambana na wizi huo na licha ya kuwakamata baadhi ya
wahalifu ambao baadhi yao walifikishwa mahakamani na kesi zao bado
zinaendelea kusikilizwa kwenye mahakama mbalimbali hapa nchini bado wizi
unafumuka kwa kasi tena ya ajabu chanzo kikuu kikitajwa kuwa ongezeko
la mahitaji. Kila
kukicha TANESCO imekuwa ikingia gharama katika kununulia vifaa
vilivyoibwa badala ya kuendeleza maendeleo ya miradi ya umeme nchini.
No comments:
Post a Comment