Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Yunus
Mgaya, amesema wanafunzi 22 waliosimamishwa, wanaandaliwa mashtaka
kuhusiana na matukio yaliyosababisha vurugu chuoni hapo.
Akizungumza n jana jijini Dar es Salaam, Profesa Mgaya alisema mashitaka hayo yatakamilika ndani ya wiki hii.
Alisema
wanafunzi hao watapewa siku saba za kujitetea na baada ya hapo itaundwa
kamati ya nidhamu ya wanafunzi ili kusikiliza utetezi wao. Profesa
Mgaya alisema chuo hakijawafukuza wanafunzi na kwamba, katika suala
hilo kuna taratibu mbalimbali, ambazo zinatakiwa kufuatwa.
Hata
hivyo, Profesa Mgaya alisema baada ya utetezi wao kusikilizwa,
itaandikwa ripoti, ambayo itakuwa na mapendekezo yatakayotumika katika
kutoa maamuzi.
Alisema kila mwanafunzi atapewa adhabu kulingana na mashitaka.
Profesa
Mgaya alisema wanafunzi 50, ambao wamefikishwa mahakamani, watano kati
yao, tayari walishasimamishwa, hivyo watakuwa wanakabiliwa na adhabu
mbili.
MWALIMU APIGWA HADI KUFA
Amar’e Stoudemire and Fabolous turned up the swagu last night as
they celebrated their birthdays together at the Catch Roof in New York.
The fellas got dapper as they celebrated with celebrity friends
Adrienne Bailon, Emily B, Rosci Diaz, Jessica White, Angela Simmons,
Trey Songz, Ryan Leslie and plenty more.
MWALIMU APIGWA HADI KUFA
Raia mmoja wa Afrika kusini
ameshtakiwa kwa mauaji baada ya kaka yake kupigwa hadi kufa mbele ya
wanafunzi wake karibu na mji wa Polokwane kaskazini mwa nchi hiyo.
Guilford Shapo, mwalimu katika shule ya msingi
ya Masehlong, alishambuliwa alipokuwa akisimamia mitihani siku ya
Jumanne, chombo cha habari cha umma cha Afrika kusini kiliripoti.
Mdogo wake wa kiume Happy Shapo ameshtakiwa kwa uhalifu huo, msemaji wa polisi Ronel Otto aliiambia BBC.
Bw Shapo hakutakiwa kusema lolote na kesi hiyo imeahirishwa hadi wiki ijayo.
Gazeti la nchi hiyo la Star lilimnukuu Noko
Moabelo, mkuu wa shule katika kijiji cha Ga-Mmasehlong kwenye jimbo la
Limpopo akisema, " Tulishtushwa na wanafunzi walipopiga kelele na
kukimbia kutoka darasani."
Alisema, "Bw Shapo alikuwa mwalimu pekee wa
kiume katika shule hiyo. Tukiwa wanawake, hakuna hata mmoja wetu ambaye
angeweza kujaribu kupambana na mshukiwa huyo."
Majirani waliosikia makelele hayo walikimbilia shuleni hapo kusimamisha mashambulio hayo ya mapanga, gazeti hili liliripoti.
Guilford Shapo alifariki dunia baadae kutokana na majeraha.
Luteni Kanali Otto alisema ombi lake la dhamana litasikilizwa Novemba 21 siku ya Jumatatu.
Idadi ya matukio ya mauaji yamepungua sana
Afrika kusini tangu kumalizika kwa enzi za ubaguzi wa rangi mwaka 1994,
lakini bado matukio hayo yanaongoza ukilinganisha na nchi nyingine baada
ya kutokea zaidi ya mauaji ya watu 40 kwa siku.
No comments:
Post a Comment