Masaa
machache baada ya Raisi wa shirikisho la soka nchini TFF, Leodgar Tenga
kuomba kukutana na viongozi wakuu wa vilabu 14 vinavyoshiriki katika
ligi kuu ya Tanzania bara kwa ajili kuzungumzia utata wa namna ya
uendeshaji wa ligi kuu ya msimu ujao utakavyokuwa, sasa taarifa za muda
huu zilizothibitishwa zinasema viongozi hao wa vilabu wamekutana jioni
katika hoteli ya Movenpick na kuamua kuwa hawatokwenda kukutana na Tenga
kesho kama alivyoomba.
Viongozi
hao wa vilabu wamesema sababu kuu ya kukataa kwenda kufanya mazungumzo
na Tenga ni kwa sababu hawadhani kwamba kuna jipya lolote wataloambiwa
ili kuweza kubadili msimamo wao wa ligi ya msimu ujao kuendeshwa na
kampuni ya vilabu.
“Hatuoni
kama kuna umuhimu wowote wa kufanya majadiliano juu ya suala hili, sisi
sote tumeshaamua kwamba msimu ujao ligi itaendeshwa na kampuni ya
vilabu vishiriki, TFF na Tenga wenyewe hawataki, wanataka kamati
itakayoteuliwa na Tenga ndio iendeshe ligi.
Tenga anataka tukae tujadili
ajenda ipi? Sisi kwa pamoja tumeshaamua kwamba ligi ya msimu ujao
itaendeshwa na kampuni yetu na huu uamuzi wetu wa mwisho,” alizungumza
Geoffrey Nyange Kaburu ambaye ni mwenyekiti wa Kamati maalum ya
kusimamia mchakato wa uanzishwaji wa Kampuni ya kusimamia ligi kuu
kuanzia msimu ujao.
TONY BRAXTON AFUNGUKA DHIDI YA KASHFA YA KUTEMBEA NA KIJANA WA MIAKA 12
TONY BRAXTON AFUNGUKA DHIDI YA KASHFA YA KUTEMBEA NA KIJANA WA MIAKA 12
Yesterday, Toni Braxton and her sisters along with their mother made
an appearance on The Wendy Williams show to promote the second season of
“The Braxton Family Values.” There was a whole lot of Braxton
personality on that stage as the sisters talked about Trina’s drinking
problems, Tamar’s lighter skin, Towanda’s open relationship with her
husband and Mama Braxton wanting to smack the p*ss out of Tamar. Toni
also discussed her health, bankruptcy and money issues as well as her
personal life. When she was asked if the rumors were true that she dated
Terrence J from 106 and Park, Toni gave a pretty blunt answer:
You know that’s not true. I think he’s a cutie but he’s young; he’s 12. He doesn’t have no money. Sorry
I guess you better show some bank statements and come correct if
you’re thinking about stepping to Toni B. She has major bills that need
to be paid. She also revealed on the show that she’s been playing ‘in
the snow’… if you catch my drift.
MTOTO WA BAKHERSA APIGA WAANDISHI WA HABARI DAR
Jamal
Bakhresa akitumia helmeti kuwapiga nayo waandishi wa habari waliodaiwa
kumpiga picha yeye na mwendesha pikipiki mwenzake walipogongana
katika Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana. Anayejaribu
kumzuia ni Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda
ambaye alipigwa na helmeti hiyo kichwani. Pembeni ni Cathbert Kajuna
ambaye ni mwandishi wa gazeti la Kitangoma linalomilikiwa na Clouds
Media ya jijini Dar es Salaam alikuwa
akijaribu kumuamulia ugomvi.
Jamal kwa kitendo chake cha kuwaingilia wakati wakiwa kazini. Vitendo
kama hivi vya kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi zao vimekuwa
vikitokea mara wa mara ambapo vimekuwa vikiwasababishia hasara ya mali
zao na vifaa kupoteza vifaa vya kazi.
UTURUKI YAPATA WAZIRI MKUU MPYA
Makamu wa zamani wa rais wa
benki ya Ulaya Lucas Papademos ametangazwa kuwa waziri mkuu mpya wa
Ugiriki, kufuatia siku kadhaa za majadiliano.
Taarifa ya kuthibitishwa kwa nafasi ya Bw Papademos imetoka katika ofisi ya rais wa Ugiriki.
Viongozi wa vyama vikuu vitatu
vinavyounda serikali ya umoja wa kitaifa wamekuwa wakikutana na rais
waUgiriki kujaribu kufikia makubaliano.
Waandishi wa habari wanasema Wagiriki watakuwa
na imani kuwa taarifa hizi zitaleta utengamano kuwasiadia kukabiliana na
janga la madeni.
Bw papademos atahitaji kuongoza serikali ya
mpito inayoundwa, kuhakikisha nchi hiyo yenye deni kubwa inapata fedha
za kuisaidia, na kuidhinisha fungu la dharura la dola bilioni 177 la
kimataifa kutoka katika nchi wanachama wanaotumia sarafu ya Euro pamoja
na Shirika la Fedha Duniani IMF.
"Rais, baada ya mapendekezo kutoka kwa viongozi
wa kisiasa waliohudhuria mkutano, wamemtaka Lucas Papademos kuunda
serikali mpya," taarifa ya ofisi ya rais imesema, baada ya mazungumzo
kati ya viongozi wa kisiasa na Bw Papademos.
Serikali mpya itaapishwa adhuhuri ya Ijumaa, amesema afisa mmoja wa ofisi ya rais.
Bw Papademos atachukua nafasi ya waziri mkuu
anayeondoka George Papandreu ambaye alitangaza kuwa anajiuzulu baada ya
kutaka kuitisha kura ya maoni kuhusu fungu la kusaidia deni kutoka eneo
la euro.
Waziri mkuu mpya atapigiwa kura ya kuwa na imani naye bungeni, siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa kituo cha TV cha serikali.
Soko la hisa la Ugiriki lilipanda ghafla baada
ya Bw Papademos kuwasili katika ikulu ya rais kuijunga na majadiliano
siku ya Alhamisi asubuhi.
No comments:
Post a Comment