MLIMA
Kilimanjaro uliopo nchini na ambao ni mrefu kupita yote barani Afrika,
umetupwa nje ya orodha ya Maajabu Saba mapya ya dunia yaliyotangazwa
juzi usiku. Taarfia
hiyo ilitolewa juzi na Eamonn Fitzgerald ambaye ni msemaji wa ‘New
Seven Wonders’ taasisi iliyokuwa ikiratibu upigaji kura kwa vivutio
vipatavyo 28 dunia nzima, vilivyoingia fainali za ‘Maajabu Saba Mapya ya
Asili.
’ Fitzgerald
alibainisha upigaji hafifu wa kura kutoka Tanzania ulishindwa kuupa
nguvu mlima Kilimanjaro ambao hata hivyo ulikuwa ukikusanya mamilioni ya
kura kutoka nchi zingine za Ulaya na Amerika kwa zaidi ya asilimia 95. Fitzgerald
ameutaja ‘Mlima Meza’ (Table Mountain) ulioko katika Jiji la Cape Town,
Afrika Kusini kuwa miongoni mwa maajabu saba mapya ya dunia.
Mlima
Meza na Kilimanjaro ndivyo vilivyokuwa vivutio pekee kutoka barani
Afrika vilivyofanikiwa kuingia kwenye fainali ya mbio hizo za kimataifa.
Hivi
sasa maajabu mapya saba ya asili ya Dunia ni pamoja na msitu mnene wa
mvua wa Amazon ulioko Amerika ya Kusini, Maporomoko ya Iguazu yaliyoko
Argentina, Kisiwa cha Jeju kilichopo Korea Kusini, Mto wa Chini ya ardhi
ujulikanao kama ‘Puerto Princesa’ ambao uko Ufilipino na Mlima Meza
(Table Mountain) wa Afrika Kusini.
BONDIA MANNY PAQUAIO AMDUNDA JUAN MANUEL KWA POINTI
BREAKING NEWZ:MGUNDUZI AFARIKI DUNIA
Evelyn Lauder, daughter-in-law of Estee
Lauder, and part-creator of the pink breast cancer symbol, passed away
yesterday from complications of nongenetic ovarian cancer. Check out the
details...
No comments:
Post a Comment