Mheshimiwa
Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi
kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha na utatuliwe kisayansi badala
ya kisiasa na pia amewapongeza machinga kwa utulivu waliouonesha bila
kupora bidhaa madukani.
Halaiki
ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara
wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika
maeneo yao ya awali, wakati utaratibu wa maeneo ya kufanyia biashara
ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.
Maelfu
ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara
wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika
maeneo yao ya awali, wakati utaratibu ukiandaliwa na halmashauri ya jiji
la Mbeya.
Jeshi
la Wananchi Tanzania(JWTZ), likiwasaidia Jeshi la Polisi kuweka hali ya
amani na utulivu mara baada ya kuisha kwa mkutano uliofanyika katika
kituo cha mabasi madogo ya abiria(daladala) eneo la Kabwe Mwanjelwa
jijini Mbeya
Wananchi
wakirudi makwao kwa furaha baada ya mgogoro uliodumu kwa siku mbili
kumalizika, baada ya hotuba ya Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini
Bwana Joseph Mbilinyi.
No comments:
Post a Comment