Miss Tanzania 2011, Salha Izrael akipunga mkono mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam jana akitokea jijini London Uingereza alikoshiriki shindano la
urembo la Dunia Novemba 6,2011.
Warembo na wanafamilia wakipiga picha ya pamoja na Miss Tanzania 2011, Salha Izrael.
Vodacom
Miss Tanzania 2011, Salha Izrael (katikati) akiwa na baadhi ya warembo
walioshiriki shindano la Miss Tanzania 2011 waliofika kumpokea katika
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana
akitokea jijini London Uingereza alikoshiriki shindano la urembo la
Dunia Novemba 6,2011. Warembo hao toka kushoto ni Jenifa Kakolaki,
Alexia Willam,Hussna Maulid na Hamisa Hussein.
Bondia Sunday Elius akipambana na Abdallah Kasimu wakati wa mashindano
ya Kova Cup Dar es salaam jana Kasimu alishinda kwa point
Bondia Mussa Mohamedi (kulia) kushoto akioneshana ufundi wa kutupa
makonde na John Christian wakati wa mashindano ya Kova Cup Dar es salaam
jana Mussa alishinda kwa point.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt.
Yassir Mohamed Ali, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es
Salaam kwa mazungumzo leo Novemba 16, 2011. Picha na Muhidin
Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Japan nchini
Tanzania, Masaki Okada, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini
Dar es Salaam kwa mazungumzo na kujitambulisha leo Novemba 16, 2011.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment