Kamati
ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetoa
onyo la mwisho kwa Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage na Ofisa Habari
wa Yanga Louis Sendeu kutokana na kutohudhuria vikao viwili mfululizo
kama walivyotakiwa na kamati hiyo.
Rage
na Sendeu wanatakiwa kujieleza mbele ya kamati hiyo iliyo chini ya
Kamishna mstaafu wa Polisi, (CP), Alfred Tibaigana, kutokana na tuhuma
za utovu wa nidhamu baada ya kudaiwa kutoa kauli zenye lengo la kushusha
maendeleo ya soka hapa nchini, wakati wa kuelekea mechi ya Ngao ya
Hisani, kati ya Simba na Yanga.
Kwa
mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, kamati hiyo
inatarajiwa kukaa hivi karibuni ambapo imeagiza Rage ataarifiwe kuwa
anayepanga vikao vya kamati hiyo sio yeye, hivyo endapo hatatokea siku
atakayoitwa, atajadiliwa na mamuzi kutolewa.
AMASHA LA STR8 MUSIC INTER COLLEGE 2011-DODOMA
Msanii Barnaba akifanya show katika tamsha la STR8 MUZIK INTER COLLEGE SPECIAL 2011 katika Viwanja vya Royal Village
NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA SIDO YA NYANDA ZA JUU KUSINI MKOANI RUKWA
Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu (MB) akikata utepe kama ishara
ya kufungua rasmi maonyesho ya 9 ya SIDO ya nyanda za juu kusini
inayoshirikisha mikoa ya Rukwa, Iringa na Mbeya. Kulia kwake
anayeshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana.
Maonyesho hayo yanafanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa
kwa kushirikisha wajasiriamali kutoka zaidi ya mikoa 14 nchini na
wengine kutoka nchi jirani za Kenya na Burundi.
Mkurugenzi
Mkuu wa SIDO nchini Ndugu Mike Laizer akifafanua jambo kwa Naibu wa
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu kwenye banda la
SIDO. Kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce
Mgana.
Uhifadhi
wa Mazingira nao umepewa kipaumbele Mkoani Rukwa, Mjasiriamali wa
uhifadhi wa Mazingira wa kikundi cha REYO akinadi miti aina mbalimbali
inayofaa kwa uhifadhi wa mazingira na matumizi mengineyo katika
maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment