Baadhi
ya washiriki wa shindano la mitindo lililojulikana kama Uni Fashion
Bash kutoka vyuo mbalimbali vya mjini Dodoma wakicheza wakati wa
utambulisho lililofanyika Royal Village Dodoma jana.
Baadhi
ya washiriki wa shindano la mitindo lililojulikana kwa Uni Fashion Bash
kutoka vyuo mbalimbali vya mjini Dodoma wakicheza wakati wa utambulisho
wa shindano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Royal Village mjini
Dodoma jana.
Mshindi
wa kwanza wa shindano la wanamitindo lililojulikana kama 'Uni Fashion
Bash',Respicious Denis (kushoto)kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
akipokea zawadi yake ya shilingi laki tano kutoka kwa mwakilishi wa TBL
kanda ya kati John Tesha, baada ya kutangazwa mshindi katika shindano
hilo lililofanyika ukumbi wa Royal Village mjini Dodoma jana.
Baadhi
ya washiriki wa shindano la ubunifuwa mavazi lililojulikana kwa Uni
Fashion Bash kutoka vyuo mbalimbali vya mjini Dodoma wakitambulishwa
jukwaani wakati wa shindano hilo.
Mshindi
wa kwanza wa ubunifu wa mavazi wa shindano la 'UNI fashion Bash' ,Irene
Rwakatale (kushoto) akipokea akipokea zawadi yake ya shilingi laki saba
kutoka kwa Meneja wa Redds, Victoria baada ya kutangazwa mshindi wa
shindano hilo jana.
Baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo malimbali vya mjini Dodoma wakishangilia wakati wa shindano hilo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo malimbali vya mjini Dodoma wakishangilia wakati wa shindano hilo.
Mwanamuziki wa kizazi kipya, Mwana FA, akishambilia jukwaa wakati wa shindano hilo.
Mwana FA, akipagawisha na mmoja wa shabiki wake jukwaani wakati wa onyesho hilo.
KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi
kufutwa kwa mashindano ya 'ALL AFRICA CUP 2011-BLANTYRE- MALAWI'
yaliyotarajiwa kuanza Novemba 22, hadi 26, 2011.
Akitangaza
mabadiliko ya safari hiyo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar
Shelukindo, alisema kuwa Pamoja na mashindano hayo kufutwa Bia ya
Safari, imeandaa ziara ya timu ya Taifa ya Pool katika mikoa ifuatayo ya
Dodoma, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga baada ya kushauriana na
chama cha mchezo huo ili kuwafanya wachezaji wa timu ya taifa kuwa
katika hali ya mchezo na kufanya mazoezi baada ya kuahirishwa kwa
mashindano hayo yaliyokuwa yafanyike Malawi.
Aidha
imeelezwa kuwa kuahirishwa kwa mashindano hayo kufanyika Malawi
kumefuatia kutokea kwa machafuko ya Kisiasa na hii itatoa nafasi kwa
mikoa iliyotajwa kuiona timu yao ya Taifa na baadhi ya wachezaji wakali
wa mikoa hiyo kupata nafasi ya kucheza na wachezaji wa timu yhiyo ya
Taifa.
RAIS JAKAYA M. KIKWETE ATUA DODOMA RASMI KUHUDHURIA VIKAO VYA CHAMA CHAKE CCM.
Katika Uwanja wa
ndege wa Dodoma Dkt Kikwete amepokewa na viongozi pamoja na wana CCM
wengi wakiongozwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Waziri
Mkuu Mizengo Pinda ambaye ni Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM.
Na Mwandishi Maalum, Dodoma, Jumamosi Nov. 19, 2011.
No comments:
Post a Comment