Rais
wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwaamulizia
mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto na Simba Watunduru
baada ya kusaini mkata wa kupambana August 30 katika ukumbi wa Diamond
Jubilee Dar es salaam.
MABONDIA
Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Simba Watunduru wamekiuka miko ya
mchezo wa masumbwi baada ya kutaka kuchapana makonde kavu kavu mbele ya
Rais wa TPBO Yassini Abdallah 'Ostadhi' wakati wa utiaji saini mkataba
wa makubaliano wa kupambana mchezo wa kirafiki August 30 katika ukumbi
wa Diamondi Jubilee.
Akizungumzia
tukio hilo rais huyo alisema sijawai kuona vitu kama hivi vya ajabu
maana vijana wamekamiana mpaka kufikia hatua ya kutaka kuchapana kavu
kavu nje ya ulingo tena mbele yangu,hata hivyo mzozo huo umekubaliana
kumalizika siku ya mpambano wao ambapo atajulikana nani mbabe zaidi ya
mwenzake.
Nae
bondia Ibrahimu Class aliyeanzisha mzozo huo ameahidi kummaliza mapema
mpinzani wake ambapo anatarajia kumchakaza raundi za awali na bondia
Simba nae ameahidi kumchapa class kwa K,O.
"Kiukweli
kabisa huyo ni kijana mdogo sana na mmemuaisha kwangu sasa siku hiyo
mimi nita mpiga K,O mbaya sana najua kuwa kwa Tanzania hii mimi ndie
naongoza kuwapiga wapinzani wangu kwa K,O pindi nikutanapo nao ulingoni"
alisema Simba.
Mpambano
huo unatarajiwa kuwa ni mkali sana na wenye mvuto wa kipekee
utakaopigwa August 30 katika ukumbi wa Diamondi Jubilee,jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment