Warembo
wanaotarajia kushiriki Redd’s Miss Ilala Talent hii leo, wakiwa wamepozi wakati wa
mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa
mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini.
**********
KATIKA
Kuelekea Redds Miss Ilala Ijumaa, leo kutakuwa na shindano la kumtafuta
mrembo mwenye kipaji (Talent) itakayofanyika katika mgahawa wa City Sports and Lounge uliopo katikati ya jiji.
Mratibu wa shindano hilo, Juma Mabakila alisema
kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza
kuwa warembo wote 14 wamejipanga kuonesha vipaji vyao ipasavyo.
Mabakila alisema mshindi wa talent atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Ijumaa ijayo katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower ulipo katikati ya jiji.
Warembo
wanaotarajia kushiriki Redd’s Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa
mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa
mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee
jijini.
Warembo
wanaotarajia kushiriki Redd’s Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa
mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa
mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini
Warembo wakiwa katika moja ya miondoko wakati wamazoezi
Mwalimu wa warembo hao, AKHSAS PETER akiwapanga vizuri kabla ya kupigwa picha na wandishi wa habari.
Warembo wakipita Mtaa wa Makunganya katikati ya Jiji la Dar es Salaam, wakitokea mazoezini katika Mgahawa wa Billicanas.
Mwandishi
Mwandamizi wa Habari za Michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula
(kulia), akitoa maelezo kuhusu kazi za kila siku za waandishi wa habari
kwa warembo wa wanaotarajia kushiriki mashindano ya Redd,s Miss Ilala
walipotembelea chumba cha habari cha Jambo Leo
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL),
Juma Pinto (aliyekaa kulia), akizungumza na warembo hao waliomtembelea
ofisini kwake, Dar es Salaam. Aliyekaa katikati ni Mratibu wa mashindano
hayo, Juma Mabakila. JCPL ni wachapishaji wa magazeti ya Jambo Leo,
Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania.
No comments:
Post a Comment