Lori lenye namba za usajili T97 AJL lenye tela namba T746 BKF lilipo acha njia na kupinduka na kuziba njia
Lori likishindwa kupita baada ya Mafuta kumwagika Barabarani na kusababisha barabara kushindwa kupitika
Askari wakijitahidi kukabiliana na watu waliokuwa wanachota mafuta
Shughuli za uokoaji zikiendelea kulia ni Dereva wa Lori hilo baada ya kunusurika
YALE
YALE!!! Wananchi wenye ndooo Haya.... Wenye Madumu haya .... wenye
Masefuria haya... wote walikuwepo kuchota Mafuta kama inavyo onekana ...
bila kujali kama yaweza kulipuka
Askari wa zima moto wakiwa wanaendelea na Juhudi za kuondoa mafuta barabarani kwa maji
Wananchi mbalimbali wakiwa wanaondoka na Mafuta... huku wengine wakiendelea kuchota
Kushoto ni Tingo Saimoni Msovela (23) na dereva wake Hassan Abdi wakijitahidi kuziba mafuta yasiendelee kuvuja
Watu
wawili wamenusurika kifo baada ya roli la mafuta lenye namba za usajili
T 978 AJL lenye tela namba T 746 BKE Aina ya SCANIA walilokuwa
wakisafiria kutoka DAR ES SALAAM kwenda ZAMBIA kuacha njia na kupinduka
katika mteremko wa MBALIZI barabara MBEYA TUNDUMA.
Dereva
ametambuliwa kwa jina la HASSAN ABDI 35 na msaidizi wake SAIMON SOVELA
23 ambao walikuwa wametokea DAR ES SALAAM kuelekea ZAMBIA likiwa limejaa
shehena ya mafuta
Kwa
mujibu wa Dereva amesema kuwa gari hilo ghafla lilipoanza kuteremka
mteremko liliharibika mfumo wa breki na mbele yake kukiwa na magari
matano baada ya kuona kuwa angesababisha maafa makubwa aliamua
kulichepusha pembeni ndipo lilipoacha njia na kupinduka na kumwaga
shehena ya mafuta.
Kikosi
cha zimamoto kilifika eneo la tukio na kuhakikisha usalama wa eneo hilo
kuhofia mlipuko wa moto ambao ungeweza kutokea kutokana na baadhi ya
wananchi kuanza kuchota mafuta yaliyokuwa yanatiririka.
Pamoja na juhudi za Jeshi la Polisi kudhibiti wananchi kutochota mafuta lakini wananchi walikaidi na kuendelea kuchota mafuta.
Ajali
hiyo ilisababisha adha kubwa kwa wasafiri waliokuwa wana pita barabara
hiyo wakiwemo wagonjwa na waliokuwa wanawahi usafiri wa ndege majira ya
saa saba mchana.
No comments:
Post a Comment