Baada
ya siku nyingi kupita tangu Shilole na Barnaba
watemane,imebainika kuwepo kwa siri kubwa zilisababisha wawili
hao watemane ....
Chanzo
cha karibu na Barnaba kimedai kuwa sababu zilizosababisha
wawili hao kutemana ni pale shilole alipodanganya umri wake
na kumwachia Barnaba jukumu la kumlelea watoto wake...
"Suala
la kulea watoto wasio wa kwake lilikuwa ni gumu sana kwa
Barnaba kwani wakati huo ndo kwanza alikuwa anaanza maisha na
hakuwa na uwezo wa kumhudumia mtu na wanae"..Kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kiliendelea kufunguka kuwa Shilole ndiye aliye mtongoza Barnaba kwa staili ya kumdanganya umri huku akimweleza kuwa swala la watoto wake lilikuwa linasimamiwa na baba yao.
Habari
zinadai kwamba, baada ya Barnaba kuingizwa mkenge, penzi lao
lilikuwa kwa kasi sana huku Shilole akijitahidi kuuficha ukweli
kwa muda mrefu.
"Cha
ajabu ni kwamba, kadri siku zilivyozidi kusonga mbele, Shilole
alijisahau na kuanza kumwachia mzigo wa kuilea familia yote..
"Aidha,
Shilole aliusahau uongo wake na akajichanganya kutoa historia
ya maisha yake katika gazeti moja la udaku ambako alitaja umri
wake halisi huku akisimulia jinsi alivyobakwa hadi kupata mimba .Jambo hilo lilimstua sana Barnaba"..Kilisema chanzo hicho na kuongeza:
"Kipengele
cha kubakwa kilimchanganya sana Barnaba akawa anajiuliza, kama
alibakwa na kupata mtoto,matunzo ya mtoto anayapataje kwa mtu
aliyembaka
"Tukio hilo lilo lilimfanya Barnaba apoteze imani na ndipo alipoanza alipoanza kutafuta visa vya kumtema Shilole"
Shilole alipotafutwa kuzungumzia suala hilo hakuweza kutoa ushirikiano wa kutosha.
No comments:
Post a Comment