MAJINA MATATU YAINGIA FAINALI “TUZO YA SHUJAA WA SAFARI LAGER”.
MAJINA MATATU YAINGIA FAINALI  
“TUZO YA SHUJAA WA SAFARI LAGER”.
Dar es Salaam, Jumatatu 03, 2011: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari  Lager na ushirikiano wa kituo cha ITV na Radio One, leo wameweka  hadharani majina matatu yaliyofanikiwa kuingia fainali za tuzo ya  “Shujaa wa Safari Lager”. Majina ya mashujaa hao ambao wanawania tuzo ya  hiyo maalum ni:-
A. MERCY SHAYO – BOMANG’OMBE, KILIMANJARO
B.  PAUL LUVINGA – SINZA E, DAR ES SALAAM
C.  LEONARD MTEPA – MWANANYAMALA A, DAR ES SALAAM
Akitangaza majina hayo,  Meneja wa Bia ya Safari Lager Fimbo Butallah alisema; “Tulipokea mapendekezo mengi toka kwa wananchi  wakipendekeza mashujaa wao na mambo waliyofanya kwa jamii, kazi  iliyofuata ilikuwa ni kupitia na kuchambua mapendekezo hayo kwa  kuangalia vigezo muhimu, ili kuweza kupata majina matatu yatakayoingia  fainali. Hatua inayofuata ni kuchapisha mambo waliyofanya mashujaa hawa  watatu katika magazeti na kutangaza katika Televisheni na Redio ili  wananchi wote waelewe na kisha waweze kupiga kura ili kuchagua shujaa  wanaetaka atwae tuzo hii ya “Shujaa wa Safari Lager 2010”.
Tunapenda kuwakumbusha wananchi wote kuwa mshindi wa tuzo  hii ya Shujaa wa Safari atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 7, pia  kutakuwa na shilingi milioni 3 ambazo zitasaidia shughuli yoyote ya  kijamii atakayopendekeza shujaa huyo mahali anakotoka. Mashujaa wawili  waliobaki wao watapata kifuta jasho cha shilingi milioni 1 kila mmoja.
GIRAFfE UNIQUE MODEL 2010
                                                      Katikati ni mshindi wa (asia dachi)UNIQUE MODELOF YEAR 2010,WPILI ALIKUWA DIANA HAMSON KULIA NA MARIAM RABII WATATU 
                                        
Tano bora ya GIRRAF UNIQUE MODEL.diana hamsin,caroline mwakasaka,mariam rabii,asia dachi na bilkis suleiman
Tano bora ya GIRRAF UNIQUE MODEL.diana hamsin,caroline mwakasaka,mariam rabii,asia dachi na bilkis suleiman
CHINA YAAHIDI KUSAIDIA SEKTA YA SANAA NCHINI
 Balozi muambata wa  utamaduni wa China, Liu Dong akifafanua jambo wakati alipomtembelea  Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego (Kulia) ofisini kwake  Ilala,Sharif Shamba wiki hii.Katikati ni wakurugenzi idara mbalimbali za  BASATA               
Katibu Mtendaji wa  BASATA,Bw.Materego akisisitiza juu ya uimarishaji wa uhusiano wa  kitamaduni kati ya China na Tanzania wakati alipopokea ugeni wa maafisa  watatu kutoka Ubalozi wa China ukiongozwa Balozi muambata wa utamaduni  Bw.Liu.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeingia kweye  makubaliano na ubalozi wa China nchini ya kubadilishana kazi za sanaa na  wasanii mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha mashirikiano ya kiutamaduni  na kukuza sekta hiyo nchini.
Akiwa katika ziara yake BASATA ambayo aliambatana na  maofisa wawili wa ubalozi wake Huang Wei na Wang Hong,Balozi muambata  wa utamaduni kutoka China,Liu Dong amesema kwamba nchi yake imejipanga  kusaidia sekta ya utamaduni nchini kwa kuwashirikisha watanzania kwenye  matamasha mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja na kujenga  miundombinu ya sekta hiyo.
Bw.Liu alikubaliana kimsingi  na BASATA katika kuimarisha mahusiano ya kiutamaduni ikiwa ni pamoja na  kuweka mikakati ya kuwezesha ubadilishanaji wa kazi za sanaa na wasanii  ili wapate fursa za kuuza kazi zao, kujitangaza na kushiriki katika  matamasha mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
“China kwa sasa inaweka  nguvu kwenye suala la kubadilishana utamaduni baina ya mataifa haya  mawili.Tunategemea kuwashirikisha wasanii wa Tanzania katika matamasha  mbalimbali tutakayoyaandaa pamoja na kuwapeleka nchini China kwa ajili  ya kuongeza na kubadilishana ujuzi” alisisitiza Liu huku akitaja sanaa  za uchongaji, filamu, uchoraji, ngoma za asili, sarakasi na nyinginezo  kuwa watazipa msisitizo.
Kwa kuanzia Balozi huyo wa  China alisema kwamba,wasanii wa Tanzania watapata nafasi ya kushiriki  matamasha na maonesho ya kuazimisha mwaka wa China ambayo yanatazamiwa  kuanza mwishoni mwa Februari mwaka 2011 ambapo pamoja na wasanii kutoka  Tanzania watakuwepo pia magwiji wa tasnia hiyo kutoka China pamoja na  waandishi wa habari maarufu.
Kwa upande wake,Katibu  Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, ziara hiyo ya  maofisa wa ubalozi wa China ambayo imekuja baada ya ile ya awali ya  maofisa wa Baraza ubalozini kwao ni yenye manufaa makubwa na italeta  tija kubwa katika tasnia ya sanaa na utamaduni kwa ujumla hasa  ukizingatia wasanii wamekuwa na uhitaji mkubwa wa maonyesho na masoko ya  kazi zao.
Alingeza kwamba,BASATA iko  tayari kusaidiana na China katika masuala mbalimbali ya ukuzaji wa sekta  ya sanaa huku akiweka wazi kwamba,uhusiano wa China na Tanzania ni wa  muda mrefu sana hivyo kuna kila sababu ya kuuendeleza na kuuimarisha  zaidi.
“Kama  kuna suala lolote mtakalohitaji tuwasaidie katika kukuza ushirikiano wa  kiutamaduni sisi tuko tayari na milango iko wazi.Bila shaka eneo hili  la mashirikiano ya kiutamaduni ni nyeti sana na hatuna budi kulipa  msukumo wa kipekee” alisisitiza Materego
 
 
No comments:
Post a Comment