Miss Utalii Tanzania 2010/11  kujizolea milioni 150
Wakati fainali za taifa za shindano la Miss  Utalii Tanzania zimepangwa kufanyika usiku wa Februari 5, 2011, mrembo  atakayenyakua taji la taifa la Miss Utalii mwaka huu ataondoka na faida  kubwa ya zawadi ya mkataba wenye thamani ya shilingi milioni mia moja na  hamsini. 
Taarifa iliyotolewa na Rais wa Miss Utalii  Tanzania, Gideon Chipungahelo imeeleza kuwa, shindano la mwaka huu  litafanyika kwenye hoteli ya kitalii ya Kiromo View Resort iliyopo  umbali wa kilometa kumi tu toka Bagamoyo mjini ambapo pia kutakuwa na  burudani kadhaa zitakazosindikiza usiku huo adhimu na ya kihistoria  katika tasnia nzima ya urembo na utalii hapa Tanzania. 
Akaendelea kusema; washiriki wote wa fainali za  Miss Utalii Tanzania 2010/11 wako katika hali nzuri kiafya na  kisaikolojia kwa ajili ya shindano na kufafanua kuwa mbali ya kitita  hicho kwa Malkia wa mwaka huu, warembo wengine wataweza kujitwalia  mataji yatakayowakilisha hifadhi za taifa 16 zilizo chini ya mamlaka ya  hifadhi za Taifa (TANAPA). 
Kadhalika, Chipungahelo amesema kuwa mbali ya  mataji ya hifadhi, pia, kutakuwa na tuzo zingine toka baadhi ya  makampuni na taasisi zilizodhamini shindano hili ili kuyawakilisha  katika suala zima la kuutangaza utalii kupitia hifadhi za taifa na  utamaduni wa Mtanzania na hivyo kuongeza hamasa zaidi kwa washiriki  ambao nao wameonesha kujawa shauku ya kufanya vema.
“Fainali za  taifa za Miss Utalii Tanzania 2010/11, zitakuwa tukio kubwa zaidi la  kitaifa la kitamaduni na urembo nchini, ambalo kishindo chake kitaleta  mageuzi makubwa katika sanaa ya urembo nchini, barani Afrika na duniani  kwa ujumla. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa mara ya kwanza dunia  itashuhudia idadi kubwa ya warembo wakiwa jukwaa moja wakitangaza na  kuonesha utamaduni kupitia mavazi ya asili, ya kitalii, ya mitindo, ya  ubunifu. Pia,  warembo hao wataonesha vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za  asili za mikoa au kanda wanazowakilisha,’ amesema Rais wa Miss Utalii  Tanzania. 
Aidha, amewataja wadhamini wakuu wa shindano la  taifa la Miss Utalii 2010/11 ni Mamlaka ya Hifadhi za Taifa  (TANAPA) ,Business Times Limited, Kiromo View Resort na Sahara Media  Group Limited,inayomiliki kituo cha runinga cha Star TV, Radio  Free Africa, Kiss FM na gazeti la Msanii Afrika. Wengine ni  Zizzou Fashion, Alaisy Travel, Auckland Tours, Tintona TankStation, Tesco  Furniture, Mlonge By Makai Enterprises,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro  (NCAA) na Coco Beach.
Warembo hao wameanza ziara rasmi za kutembelea  na kutangaza vivutio vya utalii ,kwa kutembelea maeneo ya kihistoria  yaliyopo Mkoani Pwani,ambapo juzi walitembelea Maeneo ya Kihistoria  yaliyopo wilayani Bagamoyo ikiwemo Magofu ya Kaole,wakiongozwa na katibu  tawala wa wilaya ya Bagamoyo. Aidha jana warembo wote 60 walitembelea  na kutangaza Fukwe za Bahari ya Hindi zilizoko mkoani Dar Es Salaam wakiongozwa na Mbunge wa  Kinondoni Mh, Idd Azan. wakiwa katika Fukwe wa Coco Beach warembo hao  wakiwa wamegawanywa katika timu nne za mpira wa miguu walishindana  kusakata kabumbu la Ufukweni hali iliyopelekea kuwa kivutio kikubwa na  kusababisha ufukwe huo kufurika mamia ya watu wakishuhudia warembo hao  wakionyesha vipaji vya hali ya juu ya kusakata kandanda. michuano baina  ya timu hizo za warembo zilizopewa majina ya hifadhi za Taifa ulikuwa  mkubwa na kuamsha shangwe za mara kwa mara kwa  wapenzi waliojazana kushuhudia mechi hizo. katika mchezo wa kwanza timu  ya soka ya warembo wa Ngorongoro iliweza kuibwaga timu ya soka ya  Selous kwa mabao 4-2 wakati katika mchezo wa pili ambao ulizikutanisha  timu za Serengeti National  Park dhidi ya Maunt Kilimanjaro na matokeo timu ya Mlima  Kilimanjaro kuibuka kwa ushindi wa mabao 3-1. Mbunge wa Kinondoni Mh,  Idd Azan kwa kufurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na timu hizo za  warembo wa  miss Utalii Tanzania 2010- 2011 ambao tarehe 5 mwezi wa pili  watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2010- 2011  katika Hotel ya Kitalii ya Kiromo Bagamoyo, alinunua kila goli kwa  shilingi elfu kumi(10,000) hivyo aliweza kutoa shilingi laki moja kwa  magoli kumi yaliyofungwa. naye mfanyabiashara maarufu nchini Zizzou  Fashion alitoa seti nne za jezi kwa warembo wote 60. wakati huohuo  warembo hao wanatarajia kuanza ziara ndefu ya kutembelea na kutangaza  hifadhi za taifa wakiambatana na waandishi wa  habari, wapiga picha za Video na Television huku wakitengeneza filamu  na makala ya kutangaza hifadhi hizo za taifa Kimataifa na Kitaifa katika  ziara itakayoanza jumatano hii iliyopewa jina la Tanzania Great Safari  & Tour 2010\2011 
MENGI ATOA ONYO KWA VIONGOZI WA DINI
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amewataka viongozi wa dini nchini kuacha kuhubiri kwa kutoa maneno ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mengi alisema hayo jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya chakula cha mchana na watu wenye ulemavu.
“Ninawaomba viongozi wa dini zote nchini kutohubiri kwa kutoa maneno ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwa chanzo cha kuhatarisha amani na utulivu wa nchi,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema pindi kunapotokea uvunjifu wa amani kundi la walemavu huwa la kwanza kuathirika.
Alisema amani na utulivu uliopo nchini unatakiwa kuwa endelevu ili nchi iendelee kusifiwa ndani na nje.
Aliongeza kwamba walemavu wanaweza kupata fursa sawa na kundi lingine la jamii endapo suala la amani na utulivu litazidi kushamiri nchini.
“Kwa niaba ya kundi hili na wengine wote nchini, ninatoa rai ya kuwataka kudumishwa kwa amani na utulivu nchini,” alisema Mengi.
Awali, Mwakilishi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata), Lupi Naswanya, alisema wanahitaji Katiba mpya kwa maslahi ya taifa na jamii hiyo kwa ujumla.
Lupi alisema serikali haina budi kuwashirikisha katika mchakato wa kuandaa Katiba mpya kama moja ya jamii ya Watanzania.
“Tunahitaji kushirikishwa katika mchakato wa kuandaa Katiba mpya, Katiba iliyopo inahitaji mabadiliko makubwa kutokana na kutotupa fursa sawa katika jamii,” alisema.
Aliongeza kwamba endapo Katiba itakuwa nzuri, jamii yote itaboreka, hivyo bado kunahitajika maboresho katika Katiba ya sasa,” alisema.
Mengi amekuwa na utaratibu wa kila mwaka wa kuandaa tafrija kwa ajili ya jamii ya watu wenye ulemavu na kupata nao chakula cha mchana na kubadilishana nao mawazo.
SEE MICHELLE OBAMA'S STYLE CHOICES
"My understanding," de la Renta said, "is that the visit was to promote American-Chinese trade — American products in China and Chinese products in America. Why do you wear European clothes?"
But de la Renta - who has criticised Mrs Obama's fashion choices before - insists it isn't a case of sour grapes.
"I'm not talking about my clothes, my business," he told WWD. "I'm old, and I don't need it. But there are a lot of young people, very talented people here who do."
         WITH awards season in full  swing, there was plenty of red carpet fashion moments this week. At the  Critics' Choice Awards in LA, Livia Firth showed that ethical fashion  can look as good as it is for the planet, while 12-year-old Elle Fanning  (in Valentino), Emily Blunt (in Azarro), and Tilda Swinton (in Lanvin),  also impressed us. 
MENGI ATOA ONYO KWA VIONGOZI WA DINI
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amewataka viongozi wa dini nchini kuacha kuhubiri kwa kutoa maneno ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mengi alisema hayo jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya chakula cha mchana na watu wenye ulemavu.
“Ninawaomba viongozi wa dini zote nchini kutohubiri kwa kutoa maneno ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwa chanzo cha kuhatarisha amani na utulivu wa nchi,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema pindi kunapotokea uvunjifu wa amani kundi la walemavu huwa la kwanza kuathirika.
Alisema amani na utulivu uliopo nchini unatakiwa kuwa endelevu ili nchi iendelee kusifiwa ndani na nje.
Aliongeza kwamba walemavu wanaweza kupata fursa sawa na kundi lingine la jamii endapo suala la amani na utulivu litazidi kushamiri nchini.
“Kwa niaba ya kundi hili na wengine wote nchini, ninatoa rai ya kuwataka kudumishwa kwa amani na utulivu nchini,” alisema Mengi.
Awali, Mwakilishi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata), Lupi Naswanya, alisema wanahitaji Katiba mpya kwa maslahi ya taifa na jamii hiyo kwa ujumla.
Lupi alisema serikali haina budi kuwashirikisha katika mchakato wa kuandaa Katiba mpya kama moja ya jamii ya Watanzania.
“Tunahitaji kushirikishwa katika mchakato wa kuandaa Katiba mpya, Katiba iliyopo inahitaji mabadiliko makubwa kutokana na kutotupa fursa sawa katika jamii,” alisema.
Aliongeza kwamba endapo Katiba itakuwa nzuri, jamii yote itaboreka, hivyo bado kunahitajika maboresho katika Katiba ya sasa,” alisema.
Mengi amekuwa na utaratibu wa kila mwaka wa kuandaa tafrija kwa ajili ya jamii ya watu wenye ulemavu na kupata nao chakula cha mchana na kubadilishana nao mawazo.
Don't Wear British!
OSCAR DE LA RENTA has criticised Michelle Obama for wearing an Alexander McQueen gown to the state dinner with Chinese President Hu Jintao. Obama also wore a dress and coat by London-based designer Roksanda Ilincic during the visit.SEE MICHELLE OBAMA'S STYLE CHOICES
"My understanding," de la Renta said, "is that the visit was to promote American-Chinese trade — American products in China and Chinese products in America. Why do you wear European clothes?"
But de la Renta - who has criticised Mrs Obama's fashion choices before - insists it isn't a case of sour grapes.
"I'm not talking about my clothes, my business," he told WWD. "I'm old, and I don't need it. But there are a lot of young people, very talented people here who do."
Best Dressed Of The Week - 21/01/2011
  GEMMA ARTERTON-AMERICANSEXY FASION MODEL
 
No comments:
Post a Comment