Uwanja wa ndege wa Domodedovo wa  Moscow umetikisika baada ya kutokea mlipuko wa bomu ambapo msemaji wa  uwanja huo alisema watu 35 wamefariki dunia.
Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa- 20 wakiwa katika  hali mbaya sana kutokana na mlipuko huo, ambapo ripoti zinasema  shambulio hilo limefanywa na mtu aliyejitoa mhanga.
Mchunguzi mkuu wa Urusi alisema magaidi ndio wamehusika na shambulio hilo.
Uwanja huo, ambao una shughuli nyingi katika mji mkuu wa Urusi, upo kilomita 40 kusini-mashariki mwa mji huo.
 
Mwathirika wa mlipuko wa bomu, Moscow
Rais Dmitry Medvedev alisema waliohusika na shambulio hilo watasakwa mpaka wapatikane.
Ameamuru kuwepo na usalama zaidi kwenye mji  mkuu, kwenye viwanja vya ndege na vituo vengine vya usafiri, na pia  ameitisha mkutano wa dharura na maafisa waandamizi.
Pia imebidi kuahirisha safari yake ya kuhudhuria mkutano wa uchumi duniani huko Davos.
Mwandishi wa usalama wa BBC Gordon Corera alisema mashaka moja kwa moja yataelekezwa kwa wapiganaji kutoka mji wa Caucasus.
Corera alisema, wapiganaji wanaopambana Caucasus  wanajua namna mwonekano wa Rais na waziri mkuu wa kuwa na jamii salama  ilivyo muhimu kwao, na hivyo kuutikisa usalama huo ni lengo lao kuu.
Mwezi Machi mwaka jana mfumo wa treni za chini  ya ardhi kwenye mji mkuu wa Urusi ulitikiswa na wanawake wawili  waliojitoa mhanga kutoka mji wa Dagestan, na kusababisha vifo vya watu  40  na kujeruhi zaidi ya 80.
              
FASHION MODEL
Izable Goulart is one of Victoria’s Secret  beautiful models.  This Brazilian beauty seems to be in love with  Victoria’s Secret new Bare Bronze Body-Perfecting Spray Tint: “I like to  tan all year long, so this sexy tint is my new best beauty friend.”

Brazilian Model-Izabel Goulart.
Sexy, radiant skin is always in! Introducing two new ways to get  glowing with an all-over body bronzer and shimmering fragrance mist.  Both are part of the new Victoria’s Secret Bare Bronze Collection of  glowing bronzers, daily glow moisturizers and makeup. The perfect way to  capture a sexy sun-kissed glow all year long.
 | 
 | WAGE AKILI KUMPA RUSHWA JERY MURRO  
 |  |  | 
 | 
 | SHAHIDI wa pili upande wa Jamhuri katika kesi ya kuomba rushwa ya sh milioni  10 inayomkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la (TBC1) Jerry  Murro, na wenzake Michael Wage amekiri kutoa rushwa ya sh milioni moja baada ya  kutishiwa bastola na pingu. Wage alitoa maelezo hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya  Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe wakati akiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka  nchini Boniface Stanslaus.
 Alidai kuwa alilazimika kutoa rushwa hiyo kwa sababu alitishwa na Murro na  mshtakiwa wa pili Kapama aliyejitambulisha kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa PCCB na  mshtakiwa wa tatu Deo Mgassa alijitambulisha kuwa ni msaidizi wa mkurugenzi  huyo.
 Shahidi huyo ambaye alikuwa mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo  kabla ya hajasimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Januari mwaka jana,  alidai kuwa washtakiwa hao wote watatu Januari 31 mwaka jana, katika Hoteli ya  Sea Cliff walimtaka awapatie sh milioni 10 ama sivyo wangembambikia kesi kama  alivyobambikiwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus  Liyumba, kwa kumwambukiza maradhi mpenzi wa rafiki wa Kapama ndiyo maana  akabambikiziwa kesi iliyomfanya ahukumiwe kwenda jela miaka miwili.
 Wage aliieleza Mahakama kuwa Januari 28 mwaka jana akiwa nyumbani kwake  Bagamoyo alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa mtangazaji wa TBC1  na hakuwa hakimfahamu, akimtaka kesho yake aje Dar es Salaam kwa ajili ya  mahojiano kwani amepata taarifa kuwa anakabiliwa na tuhuma za ufisadi katika  Halmashauri ya Bagamoyo.
 Katika hilo Wage alieleza kuwa alikubaliana na ombi hilo na Januari 29 mwaka  jana, saa tano asubuhi alifikia katika mgahawa wa Califonia ulioko jijini hapa  akiwa na dereva wake.
 Alisema akiwa njiani alimpigia simu Murro ili aje aungane naye na baada ya  dakika chache Murro aliwasili katika mgahawa huo akiwa na gari ndogo na  akamweleza watafute meza nyingine ili wakae mbali na dereva wake na walipohamia  kwenye meza nyingine ndipo Murro alipoanza kumueleza tuhuma za ufisadi  zinazomkabili na kwamba anataka kuzitangaza kwenye kipindi cha Usiku wa Habari  kinachorushwa na TBC1.
 “Baada ya Murro kunieleza tuhuma hizo akaniambia mahojiano kamili  yangefanyika katika Hoteli ya Sea Cliff kwani huko ndiko walikokuwa mabosi wake  na kunitaka nimwache dereva wangu kwenye mgahawa huo nikapande gari lake twende  nae Sea Cliff na nilifanya kama alivyonielekeza nikapanda na tulipokuwa njiani  akampigia simu mtu akawa anazungumza naye na akanitaja jina langu… alivyokata  simu nikamuuliza ni kwa nini alikuwa akitaja jina langu akasema alikuwa  akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa PCCB (Kapama) naye pia atanihoji.
 “Kitu kingine wakati nilipokuwa ndani ya gari hilo tukielekea Sea Cliff,  Murro aliniambia yeye ni ofisa wa jeshi na ana nyota tatu na amechukua mafunzo  nchini Marekani na Afrika Kusini na ana madaraka ya kunikamata… na baada ya hapo  alifungua dashibodi ya gari lake akatoa pingu akaniambia nikimletea vurugu  atanifunga na pingu na kisha akanionyeshea bastola pia akaniambia nikifanya  vurugu atanifyatulia risasi ili kunidhibiti,” alieleza.
 Wage aliendelea kueleza kuwa walipofika tu Hoteli ya Sea Cliff walipokelewa  na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa PCCB, anaitwa Mussa ambapo  hata hivyo Wage alimtambua mtu huyo mahakamani kuwa ni Mugassa na akaongeza mtu  mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Dokta ambaye Wage jana alimtambua  mahakamani kuwa ni Kapama na kuongeza kuwa baada ya hapo mahojiano yakaanza na  Dokta akaanza kumueleza kuwa yeye ni fisadi mkubwa na kwamba kama alihitaji  msaada wao angesema mapema ili mahojiano yao yasiweze kurushwa kwenye kipindi  cha Usiku wa Habari cha TBC1.
 “Niliwajibu mimi siyo fisadi; ndipo yule Dokta (mshtakiwa wa pili) akaniambia  kuwa hata Liyumba alifungwa jela kwa kuonewa kwani ile kesi ya matumuzi mabaya  ya ofisi ya umma, alibambikiziwa kwa kuwa alikuwa akitembea na mpenzi wa rafiki  yake anayefanya kazi BoT akamwambukiza maradhi… nilipokea taarifa hiyo kwa  mshtuko mkubwa na nikaona wanaweza kunibambika kesi watu hao na siku hiyo  nilikuwa na sh milioni moja mfukoni ikabidi nimpatie kiasi hicho cha fedha Kaimu  Mkurugenzi wa PCCB (Kapama), mshtakiwa wa pili, ndani ya gari na Murro alikuwa  nje ya gari na kuwaahidi kesho yake Januari 31 mwaka jana ningewaletea sh  milioni tisa zilizokuwa zimebaki.
 “Baada ya kumaliza kuwapatia sh milioni moja, niliingia kwenye gari la Murro  akaenda kunishusha mgahawa wa Best Bite na tutakubaliana kesho yake tukutane  kwenye mgahawa wa City Garden ulioko mtaa wa Mkwepu… Nikapanda kwenye gari langu  nikaenda nyumbani kwangu Bagamoyo nikawaeleza ndugu zangu kuhusu tukio la mimi  kutishiwa bastora na kuombwa rushwa; wakaniambia nikatoe taarifa polisi….na  kweli Januari 31 mwaka jana, nilivyokuja Dar es Salaam nilifikia moja kwa moja  kituo kikuu cha Polisi Kati huku mfukoni nikiwa na sh milioni tisa,” alidai  Wage.
 Alisema mara baada ya kutoa taarifa hizo polisi wakamtaka ampigie simu Murro  na amweleze kuwa tayari ameishafika kwenye mgahawa wa City Garden.
 Wage alieleza kuwa alifanya hivyo na baada ya dakika chache Murro aliwasili  kwenye mgahawa huo lakini alivyomuona Wage ameambatana na watu wengine watatu  alishtuka na polisi waliwahi kuzuia gari lake lisitoke katika viwanja vya  mgahawa huo na askari kanzu hao walimwamuru aendeshe gari lake na kulipeleka  kituo cha polisi Kati na Murro alitii amri hiyo na wote walifika kituoni hapo.
 Alisema Murro alipoulizwa kama alikuwa akimfahamu Wage alikana kumfahamu na  polisi hao walipopekuwa gari la Murro walikuta bastola, pingu na miwani ya  kusomea ambayo Wage alidai ni yake na aliisahau jana yake wakati alipopanda  katika gari hilo wakati anapelekwa Sea Cliff.
 Vitu hivyo vyote pingu, bastola na miwani ilipokelewa mahakamani hapo kama  utambulisho. Kwa upande wake wakili wa Murro, Richard Rweyongeza, na Majura  Magafu, anayemtetea Kapama na Muggasa akimhoji shahidi huyo alidai kuwa shahidi  huyo haoni kwamba Murro alikuwa akitangaza habari za hatari hatari za kuligusa  jeshi la polisi na alikuwa akitaka kurusha tuhuma za ufisadi zinazomkabili Wage  ndiyo maana alishirikiana na polisi kumbambikizia kesi mteja wake, hoja hiyo  ilipingwa vikali na shahidi huyo. Leo shahidi wa tatu atahojiwa.
 
 
 |  | 
No comments:
Post a Comment