Klabu
ya Simba ya Dar es Salaam leo imekubali kipigo kutoka kwa Villa SQUAD
katika mfulululizo wa ngwe ya lala salama ya Vodacom Premier League.
Katika
mchezo huo uliofanyika jijini DSM katika uwanja wa taifa Villa
ilifanikiwa kuondoka na pointi 3 baada ya kuibuka na ushindi wa goli
1-0.
Villa ambao walimaliza mchezo huo wakiwa 10 dimbani walifunga goli lao katika dakika ya 40 likiwekwa kimiani na Nsa Job.
Katika
hatua nyingine Coastal Union ya Tanga imeendeleza wimbi la ushindi
baada ya kuifunga Moro United 1-0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja
wa Chamazi – Dar es Salaam. Goli la Coastal lilitiwa kimiani na Rashid
Yusuf katika kipindi cha pili.
No comments:
Post a Comment