Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA,Mh Zitto Kabwe
Inasikitisha
kwamba Bunge laweza kukaa wiki nzima na kujadili masuala mbalimbali
bila kutoa muda kujadili suala la mtikisiko katika sekta Afya.
Siku ya kwanza ya Bunge nilisimama kutaka taarifa ya serikali kuhusu
mgomo wa madaktari na taarifa hiyo ijadiliwe na Bunge. Spika
akalojulisha Bunge kwamba Serikali imempa taarifa na itawasilishwa.
Bunge lika...ahirishwa
siku bila kurejea. Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipohitaji taarifa ya
Serikali, Serikali haikuwa na taarifa. Kwa hiyo walifanya ujanja ujanja
kuzuia mjadala wa mgomo wa madaktari.
Leo wabunge kwa mara nyingine wamesimama kutaka mjadala huu wa dharura.
Naibu Spika wa Bunge akatumia sababu za kiufundi kuzuia mjadala.
Inawezekana wabunge hawakuwaandaa wabunge kusimama kuunga mkono hoja,
lakini ni jukumu la Kiti kuona umuhimu na udharura wa mijadala.
Hii inadhihirisha kwamba sasa Bunge kama Mbunge mmoja mmoja au kwa
ujumla wake na Taasisi ya Bunge imekosa mguso na Hali ya wananchi (out
of touch). Hali hii ni hatari sana. Wananchi wanapoona chombo
kinachowawakilisha hakitoi nafasi kwa masuala yanayowagusa, watachukua
hatua zao wao wenyewe na hivyo kuhatarisha utulivu wa nchi. Bunge liache
shughuli nyingine zote na kutoa fursa ya kupokea taarifa ya serikali
kuhusu madai ya Madaktari, kuijadili na kuazimia kwa kuelekeza hatua za
kutekelezwa na serikali.
No comments:
Post a Comment