MAMIA
wafurika kushuhudia hukumu ya msanii nyota wa muziki wa kizazi
kipya nchini Naseeb Abdul a.k.a Diamond akihukumiwa kifungo cha miezi
sita jela au kulipa faini ya shilingi elfu 50.000 kwa kosa la
kumshambulia na kuharibu mali za mwandishi wa habari mkoani
Iringa Francis Godwi.
Hatua
hiyo imekuja baada ya msanii Diamond na wacheza shoo wake wawili kukiri
kosa mbele ya mahakama yeye na wenzake kwa kuharibu Camera mbili, Lap
top aina ya Accer pamoja na kumshambulia mwanahabari Francis Godwin
Desemba 31 mwaka jana katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
Akitoa hukumu hiyo hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Hakimu Masua alisema
kulingana na watuhumiwa wote watatu kukiri kosa hilo anawahukumu kwenda
jela miezi 6 au kulipa fidia ya shilingi elfu hamsini kila mmoja na huku
wakilazimika kumlipa Godwin shilingi elfu 30 kila mmoja na kufanya
kufikia kiasi cha shilingi 90000 Wakitoa utetezi wao
watuhumiwa hao walisema mahakama iwapunguzia adhabu kwa kuwa
hawakukusudia kufanya kosa hilo, na wao walikuja mkoani hapa kwa ajili
ya kutoa burudani, na kuwa tukio hilo wamelifanya kwa ghadhabu.
Mheshimiwa
Hakimu ninaomba unipunguzie adhabu licha ya kutenda kosa hilo, kwani
nakili kuwa nilipatwa na hasira kama binadamu na kuamua kuchukua uamuzi
wa kufanya hayo, mimi sikukusudia kuja Iringa kufanya vurugu bali hali
hiyo ilikuja baada ya kupata ghadhabu kama walivyo binadamu wengine,”
alisema Diamond.
Naye
mwanasheria Evaristo Myovela alisema kesi hiyo hakimu ametimiza wajibu
wake, huku akimshauri Francis kukata rufaa kama hajaridhika na maamuzi
ili kuipeleka kesi hiyo katika Mahakama nyingine kwa kufuata utaratibu
wa sheria katika kuchukua maamuzi hayo.
Wakati wanahabari wakijadili juu ya hukumu ya Diamond , mara
Waziri wa sera na uratibu wa sheria za bunge Willium Lukuvi alikatiza
katika mahakama hiyo ndipo wanahabari wakataka kupata mawazo na uelewa
zaidi juu ya hukumu hiyo.
No comments:
Post a Comment