Wakazi
wa Wilaya ya Geita mkoani Mwanza, wakiangalia mwili wa mtu
anayesadikiwa kuwa ni jambazi (jina hajafahamika), akiwa ni mmoja wa
watu wanne waliyovamia mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), akiwa amekufa
baada ya kupigwa risasi na askari polisi katika jaribio hilo la kutka
kupora dhahabu
WATU
wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia mgodi wa dhahabu wa Geita
(GGM), na kuteka ndege ya kubeba madini hayo na kupora vitofali 68 vya
dhahabu iliyokuwa ikisafirishwa kutoka mgodi huo kwenda nje ya nchi
yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 130.
Hata
hivyo, majambazi hao walishindwa kuondoka na dhahabu hiyo baada ya
polisi wilayani hapa kuwahi kufika eneo la tukio na kuiokoa, baada ya
kupambana na majambazi hao kwa kurushiana risasi na kuua mmoja.
Dhahabu
iliyonusurika kuporwa na majambazi hao kwa mujibu wa madai ya mmoja wa
polisi aliyeikagua ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, ilikuwa
ni zaidi ya kilo 1,000.
Polisi
huyo alidai kuwa dhahabu hiyo ilikuwa imegawanywa katika makasha 16
huku kila kasha likiwa na vitofali vinne vya dhahabu na kila kitofali
kikiwa na uzito wa kilo 25.
Hata
hivyo, Ofisa Madini mkazi wa Kanda ya Geita, Juma Sementa, ambaye ofisi
yake imekuwa ikikagua na kuhakiki dhahabu kabla ya kusafirishwa kila
wiki na mgodi huo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu uzito kamili wa
dhahabu iliyokaguliwa na ofisi yake juzi kabla ya kusafirishwa jana,
alitofautiana na madai ya polisi.
Sementa
alisema ofisi yake ilikagua makasha 25 na kila kasha likiwa na kitofali
kimoja cha dhahabu chenye uzito wa kati ya kilo tano na 30.
Katika
tukio hilo la aina yake, polisi walimuua mtuhumiwa mmoja baada ya
kummiminia risasi kifuani, ingawa tayari alikuwa amejeruhiwa na mmoja wa
walinzi wa mgodi huo ambaye ni raia wa Afrika Kusini.
Tukio
hilo lilitokea jana saa 5.55 adhuhuri katika uwanja wa ndege wa mgodi
huo ulioko umbali wa kilometa tano kutoka katikati ya mji wa Geita.
Kwa
mujibu wa habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa
na baadhi ya maofisa wa polisi wilayani hapa, uchunguzi wa awali
ulionesha kuwa majambazi wapatao wanne walivamia mgodi huo wakiingilia
lango kuu la uwanja huo wa ndege.
Ilielezwa
kuwa majambazi hao wakiwa na mabomu ya kutupa kwa mkono, bunduki aina
ya SMG na bastola, waliishambulia kwa risasi ndege iliyokuwa ikipakia
dhahabu kutoka kwenye gari maalumu.
“Hali
hiyo iliwafanya walinzi wa mgodi huo waliokuwa wakilinda usalama wa
mali iliyokuwa ikisafirishwa, kutimua mbio, lakini alibaki Mzungu raia
wa Afrika Kusini mfanyakazi wa mgodi huo, aliyekuwa na bastola.
“Raia
huyo wa Afrika Kusini alipambana na majambazi hao kwa kuwafyatulia
risasi,’’ alisema mmoja wa maofisa wa Polisi katika mahojiano maalumu na
gazeti hili.
Ilidaiwa
kuwa wakati raia huyo akiendelea kufyatuliana risasi na mmoja wa
majambazi hao, aliishiwa risasi na kujeruhiwa kwa kupigwa risasi kwenye
mkono na kukimbia kuokoa maisha yake.
Hata
hivyo, baada ya muda mfupi, inadaiwa askari Polisi walifika na
kupambana na majambazi hao ambapo watatu walitimua mbio na kubaki mmoja
ambaye tayari alikuwa amejeruhiwa na Mzungu huyo, akashambuliana kwa risasi na polisi, lakini alizidiwa na kuuawa na risasi za Bastola, mabomu, bunduki
Jambazi
aliyeuawa bado hajatambuliwa jina na alikutwa na bastola aina ya
Chenese namba 0048467 ikiwa na risasi sita, na bunduki aina ya SMG namba
UA89381997 inayoonekana kusajiliwa Uganda.
Pia
alikutwa na mabomu manne ya kutupa kwa mkono, magazini nne na risasi 60
ambazo hazijatumika, huku akiwa amevalia nguo za kawaida nguo nne ndani
na ya juu ikiwa ni sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ).
Jambazi
huyo naye alimjeruhi kwa risasi mfanyakazi mwingine wa mgodi huo, raia
wa Afrika Kusini aliyetambuliwa kwa jina la Engenas Van Der Schuffs,
baada ya kumpiga risasi kwenye mkono wa kulia.
Marubani wa ndege iliyoshambuliwa yenye namba SH-TZX walitambuliwa kwa majina ya Meja Kondo Hamza na Hamdan Salehe.
Hata
hivyo, habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio zilisema ndege hiyo
ilishindwa kuondoka kwenye uwanja huo kutokana na moja ya mabawa yake
kutobolewa kwa risasi.
No comments:
Post a Comment