Michuano ya mpira wa ukutani (Squash) ya kutafuta mshindi wa miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar itaanza kutimua vumbi Ijumaa wiki hii Januari 13, 2012 kwenye uwanja wa Polisi Ziwani mjini Zanzibar.
Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amemkariri Katibu Mkuu wa Chama cha Squash Zanzibar (ZSRA) (Zanzibar Squash Racket Association) Haji
Uzia Vuai, akisema kuwa michuano hiyo itawashirikishi jumla ya
wachezaji 30 wakiwemo 15 kutoka Tanzania Bara na wengine 15 kutoka
Visiwani Zanzibar.
Vuai
amesema michuano hiyo ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka wakati wa
sherehe za Mapinduzi, itafungwa Jumapili ijayo Januari 15, 2012 kwenye
uwanja wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar na Mohammed Radha.
Amesema
mshindi wa kwanza wa michuano hiyo atapata shilingi 200,000, wa pili
atapewa shilingi 150,000 na shilingi 100,000 kwa mshindi wa tatu zawadi
ambazo amesema zitatolewa na baraza la Michezo la Zanzibar.
Vuai
amesema mchezo huo una viwanja viwili tu hapa Zanzibar ambavyo kwa
kawaida vinakuwa ndani ya jengo tofauti na viwanja vya michezo mingine.
Viwanja hivyo ni kile cha Polisi Ziwani na kiwanja kilichopo kwenye
Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
Amewaomba
Wananchi mbalimbali wakiwemo wapenzi wa michezo kufika kwa wingi
kwenye viwanja hivyo vya SQUASH ili kuona na hata kujifunza sheria na
taratibu za mchezo huo.
Vuai
amesema kama ilivyo kwa michezo ya ngumi, riadha, kulusha tufe, mkuki
ama kuruka juu na chini, ushindi wa mpira wa ukutani nao unategemea
sana juhudi za mchezaji mmoja mmoja wa mchezo huo tofauti
na mpira wa miguu ama wa wavu kuwa hata kama mfungaji atakuwa mmoja
ama wawili ushindi ni wa timu nzima.
No comments:
Post a Comment