Thierry Henry amekamilisha uhamisho wa muda mfupi kurudi Arsenal.
The
Gunners wamekamilisha makubaliano ya bima na New York Red Bulls, kwa
maana Henry sasa anaweza kuanza kuichezea Arsenal kuanzia Jumatatu
katika raundi ya Kombe la FA dhidi ya Leeds.
The
34-year amesajiliwa kama mbadala wa Gervinho na Maroune Chamakh, ambao
watakuwa wakielekea Africa kucheza CAN na timu zao za taifa Morocco na
Ivory Coast.
Henry alisema: “Ni vigumu kuwa mkweli lakini linapokuja suala la Arsenal moyo ndio utakaokuwa unaongea.
“Tangu
nilipojua the plan nyuma ya usajili wangu nilikuwa sawa na kurudi
Gunners. Sijarudi Arsenal ili kuwa shujaa au ku-prove kitu chochote.
Nimerudi kusaidia tu.
“Watu wanabidi waelewe kwamba Chamakh na Gervinho wanaenda kucheza CAN, hivyo niliitwa kuja kujaza gap waliyoiacha.”
Henry atavaa jezi namba 12 mpaka atakapomaliza mkataba wake wa miezi miwili.
Welcome The Greatest King Theirry Henry.
No comments:
Post a Comment