Naibu
Waziri wa Uchukuzi Athumani Mfutakamba amesema usafiri wa reli ya kati
uliokuwa umesitshwa kwa muda unatarajiwa kurejea tena baada ya kazi ya
matengenezo ya maeneo yaliyoharibiwa na mvua katika stesheni ya Gulwe na
Godegode kukamilika kwa asilimia 80.
Dk
Mfutakamba alieleza hayo wakati akizungumza na uongozi wa reli ya TRL
karakana ya Morogoro mara baada ya kutembelea karakana hiyo kuona
shughuli mbalimbali za utengenezaji na ufufuaji wa injini za treni
ukiendelea.
Dk.
Athumani Mfutakamba alifanya ziara hiyo baada ya Uongozi wa Kampuni ya
Reli Tanzania (TRL) kufanya zoezi la kuwarejeshea nauli zao wasafiri
wapatao 1920 ambao walikuwa wasafiri na treni kutoka Dar kwenda Kigoma
siku za Jumamosi Jan 07, 2012 na Jumanne Jan 10, 2012 ambazo
zimelazimika kufutwa baada ya reli ya kati kuharibika.
Ambapo
pamoja na mambo mengine alisisistiza umuhimu wa wahandisi wa karakana
hiyo ya TRL kuharakisha ufufuaji wa injini kutokana na uhitaji mkubwa
uliopo wa ubebaji wa mizigo na abiria kwa gharama nafuu katika reli hiyo
ya kati kwa wakazi wa mikoa ya Tabora na Mwanza.
Pia
aliwataka wataalamu hao wa TRL kutumia vipuri vya ndani ya nchi kwa
kushirikiana na shirika la mzinga na mang'ulaili kupunguza gharama
badala ya kuagiza kutoka nje.
Kwa
upande wake meneja wa karakana ya TRL Morogoro mhandisi Ngosa
Ngosomwile alisema kuwa tayari serikali imeipatia kiasi cha shilingi
bilioni 4.2 kwa kupitia kampuni ya kusimamia mali za shirika la reli
RAHCO kwaajili ya matengenezo ya injini 5 na kununua vipuri vya magari
yanayoendelea na kazi.
Aidha ameomba vipuri vinavyoshikiliwa na RAHCO wapatiwe ili viweze kutumika katika kukarabati baadhi ya injini.
No comments:
Post a Comment