Mbunge
wa Kigoma Kusini (NCCR), David Kafulila, ambaye yuko kwenye mzozo na
chama chake kilichomfukuza uanachama, alisema kinachosumbua kwa sasa ni
kukosekana kwa mfumo wenye usawa wa ulipaji mishahara na posho ndani ya
serikali. Kafulila
alisema ni aibu kuona daktari akilipwa mshahara wa Sh. 900,000, lakini
wapo maofisa wadogo tu katika mashirika ya umma kama Benki Kuu (BoT) au
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanachota hadi milioni saba kwa mwezi. “Angalia
Gavana wa Benki Kuu analipwa mshahara wa Sh. milioni 20, Mkurugenzi wa
NSSF Sh. milioni 18, mbunge Sh. milioni 1.8, daktari Sh. 900,000,”
alisema na kuhoji hapa haki iko wapi. Aliongeza
kwamba waziri akisafiri nje ya nchi posho yake kwa siku ni Dola za
Marekani 420 (sawa na Sh. 672,000) lakini Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika
lililo chini yake anachota Dola za Marekani 800 (Sh. 1,280,000) kwa
siku.
No comments:
Post a Comment