Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel
Tanzania Bw, Levi Nyakundi alisema “ ulimwengu wa leo matumizi ya huduma
za intaneti/data au mtandao hayaepukiki, ukitaka kujua kinachoendelea
duniani kwa haraka basi intaneti ndio suluhisho au jawabu
linapopatikana, lakini kumekua na changamoto nyingi sana hasa pale
tunapohitaji intaneti bora ya kutuwezesha kufanya fasta mawasiliano na
tuwapendao au tunapotaka kuunganishwa na taarifa za mambo muhimu
yanayoendelea dunia kote, inawezekana kila wakati umekua ukijiuliza ni
MB au GB au kifurushi gani kitakuwezesha kufanya mambo yako kuwa poa
zaidi, hili ndilo lililotusukuma Airtel kukuletea wewe mteja wetu huduma
hii ya kisasa na ndio maana tunakuambia SWITCH ON”
“Ukiwa na Airtel ‘SWITCH ON’
watumiaji wa huduma za Intaneti Tanzania sasa wanakila sababu
yakufurahia kujipatia huduma bora zaidi kwa gharama nafuu na kufanya
chaguo la kufurushi utakacho MAALUM kwa simu yako. Hii ni huduma
inayoenda na wakati, inazingatia utamaduni wetu kwa kuwa ni ya
kukutoshelezea hitaji lako, na gharama ni nafuu kuliko zote huku
ikikuhakikishia mteja Non-stop intaneti - yaani fulu makamuzi kwa wewe
mtumiaji kutokupimiwa. Huduma hii ya pia inamuwezesha mteja kuwa na
chaguo la kifurushi iwe kwa SIKU, WIKI au MWEZI”
“Airtel
Tanzania tumejipanga zaidi kuhakikisha tunaendelea kuwa wabunifu na
kuwapatia huduma bora ya mawasiliano ya internet. Tutaendelea
kufanikisha hili kwakuwa Airtel Yatosha, Airtel Money nusu gharama, au
Bure Pack ni vielelezo vya huduma bora na nafuu tunazowapatia wateja
wetu kwa sasa na kuwafaidisha wateja kila siku.
Hivyo leo hii SWITCH ON
nimuendelezo wa kuwahudumia watumiaji wa Internet nchini Tanzania kwa
kuwapa wanachokitaka bila kikwazo yaani Fulu makamuzi” aliongeza
Nyakundi
Kwa
upande wake Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo akielezea jinsi ya
kutumia huduma hiyo alisema “Ni rahisi sana mteja wetu kujiunga,
unatakiwa tu kupiga *148*22# ikiwa tu una simu yako yenye uwezo wa
kutumia intaneti /Data kisha utaweza kujichagulia aina ya kifurushi
kinachokufaa kutokana na mahitaji yako kwa kuwa vifurushi ni maalum kwa
simu au kifaa utakachotumia yaani iwe unasimu ya Feature phone, au Simu
mpapaso (Smart phone au Tablet sisi Airtel tumekuwekea kifurishi cha
intaneti maalum kwa kila simu”
‘Vilevile
kwa wale wateja wote wa Airtel wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha pia
bado wananafasi ya kujiunga na vifurushi vya intaneti vya Yatosha na
ikiwa wamemaliza Data /intaneti na wanapenda kujiunga na Data pekee basi
wanaweza pia KU-SWITCH ON na kuendela na makamuzi” alimalizia kusema
Prisca
PICHANI JUU:
Mabalozi wa Huduma mpya ya Airtel ya ‘SWITCH ON’
wasanii maarufu Ney wa Mitego, Vannessa Mdee na Barnabas wakiwa
wameshikilia mabango yenye kuonyesha namba ya kujiunga na huduma hiyo ya
intaneti wakati wa hafla ya uzinduzi wake uliofanyika jana usiku kwenye
kiota cha Maraha cha Club Rouge ndani ya Hoteli ya Hyatt Agengy The
Kilimanjaro,Jijini Dar es Salaam.
Msaanii maarufu kwa kumiliki jukwaa na balozi wa huduma ya Airtel SWITCH ON Vanesa Mdee akiwa na wacheza shoo waki wakitoa burudani kali kwa wageni waalikwa waliohudhulia hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel kwa watumiaji wa Internet hapa nchini ijulikanayo kama SWITCH ON. hafla ya uzinduzi ilifanyika jana usiku katika Hoteli ya Hyatt Agengy The Kilimanjaro, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Airtel Tanzania, Levi Nyakundi akizungumza na wadau mbali
mbali (hawapo pichani) waliohudhulia hafla hiyo ya uzinduzi wa huduma
mpya ya Airtel kwa watumiaji wa Internet hapa nchini ijulikanayo kama
SWITCH ON. hafla ya uzinduzi ilifanyika jana usiku katika Hoteli ya Hyatt Agengy The Kilimanjaro,Jijini Dar es Salaam.
CHINI: Msaanii maarufu na mwenye uwezo
wa kutumia gitaa na kuimba pia ni Balozi wa Airtel SWITCH ON barnabas
akitoa burudani kali kwa wageni waalikwa
No comments:
Post a Comment