Mchezaji wa Golf wa Klabu ya TPDF Lugalo, Foti Gwebe akicheza wakati wa mashindano ya mchezo huo ulioshirikisha wateja wa BancABC na baadhi ya wachezaji wa Lugalo Klabyaliyofanyika Dar es Salam jana. |
WACHEZAJI
14 kati ya 52 wa mchezo wa gofu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao mwishoni
mwa wiki walishiriki mashindano ya mchezo huo yaliyojulikana kama 'Siku
ya Gofu', waliibuka kidedea baada ya kufanya vizuri katika mashindano
hayo yaliyodhaminiwa na BancABC.
Mashindano hayo ambayo yalidhaminiwa na BancABC, yalifanyikia kwenye viwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao ambao walizawadiwa vifaa mbalimbali vya kuchezea mchezo huo ni Peter Fiwa, Moses Namuhisa, Shaban Kibuna, Japhet Masai, Mohabe.
Wachezaji hao ambao walizawadiwa vifaa mbalimbali vya kuchezea mchezo huo ni Peter Fiwa, Moses Namuhisa, Shaban Kibuna, Japhet Masai, Mohabe.
Nyirabu, Joseph Tango, Hitesh Valambia na Gabriel Abel, Olimpia Flaten, F.Gwebe, A.Khamis, Rotsh, S.Denis na g.Kasiga.
Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi,mkurugenzi
mtendaji wa benki hiyo, Boniface Nyoni alisema wameamua kudhamini
mashindano hayo kutokana na kuwa wadau wakubwa wa michezo nchini.
Nyoni
alisema udhamini wao wa mashindano hayo kwa mwaka huu si mwanzo bali
ataendelea kuyadhamini kila mwaka ili kuweza kuuendeleza mchezo huo
nchini.
Alisema udhamini wao si kwenye mchezo wa gofu pekee bali ni katika michezo mbalimbali ikiwemo na soka.
Naye mmoja wa wachezaji walioshiriki mashindano hayo, George Nyakundi
aliipongeza benki hiyo kwa kuamua kudhamini mashindano hayo na kuomba
udhamini huo kutoishia mwaka huu.
"Kwa kweli sisi wachezaji wa mchezo wa gofu hatuna budi kupongeza udhamini huu,hivyo na benki nyinge pamoaja na makampuni mengine yaige mfano huu,"alisema Nyakundi
"Kwa kweli sisi wachezaji wa mchezo wa gofu hatuna budi kupongeza udhamini huu,hivyo na benki nyinge pamoaja na makampuni mengine yaige mfano huu,"alisema Nyakundi
No comments:
Post a Comment