Ni matukio nadra kutokea katika maisha, lakini haya ndiyo
yaliyomkuta Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata, baada ya kuugua
ghafla saa 36 kabla ya harusi yake.
Kuugua kwa bibi harusi huyo mtarajiwa, kumezua
gumzo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na maeneo mengine nchini,
kutokana na kile kilichoelezwa kwamba harusi hiyo ilipangwa kuwa ya
kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni
Kamata ilikuwa afunge ndoa leo katika Kanisa
Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza Dar es Salaam
na tayari kadi za mialiko zilishasambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo
wabunge.
Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake, aliugua usiku wa kuamkia jana na kupelekwa katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea ambapo amelazwa.
“Niliugua tumbo ghafla, nilipata maumivu makali
sana nikampigia daktari wangu na nilipomweleza jinsi ninavyojisikia,
aliniambia niende hospitali haraka na kutokana na hali ilivyo, waliamua
nilazwe,” alisema Kamata akiwa kitandani katika hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment