Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limepiga marufuku ngoma za kitamaduni ambazo zimekuwa zikifanyika nyakati za usiku kwenye maeneo mbalimbali Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa kukabiliana makundi ya kihalifu ambayo yamekua tishio kwa usalama wa raia.
Kufuatia kuibuka kwa makundi ya kihalifu kama Panya road na Mbwa
mwitu ambayo wengi wao wanahusishwa na ngoma hiyo kwenye uporaji na
upigaji wa watu, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam
Suleiman Kova anasema "Ni marufuku kwa ngoma yeyote ya asili kuchezwa
nyakati za usiku"
Kamanda
Kova anasema kufuatia operesheni inayoendeshwa dhidi ya vikundi hivyo
vya kihalifu, mpaka sasa tayari wanawashikilia wafuasi zaidi ya 100
ambapo pia watu wengi wamekuwa wakilalamikia vitendo viovu
vinavyofanyika nyakati za usiku wakati wa ngoma hizo maarufu kama
‘vigodoro’ pamoja na ‘baikoko'.
No comments:
Post a Comment