Taarifa zilizopatikana ndani ya
jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu makini zinadai kwamba mlalamikaji huyo
alifika kituoni hapo Jumatatu iliyopita muda wa mchana na kufungua kesi
yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi Na.
TBT/IR/1865/2014 akidai kufanyiwa unyama huo kwa siku mbili (Ijumaa
na Jumapili) wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar.
Ilidaiwa kuwa, Ijumaa iliyopita
mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na Jumapili
ilidaiwa alitekeleza ukatili wake huo ndani ya gari lake hali ambayo
ilimfanya mlalamikaji kutoa taarifa Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma
jijini Dar.
Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha anayetafutwa na polisi kwa kosa la ubakaji.
Iliendelea kudaiwa kuwa, kufuatia
maumivu makali aliyoyapata mlalamikaji huyo ilibidi aende Hospitali
ya Amana na kugundulika kuwa aliingiliwa kimapenzi na kumsababishia
michubuko sehemu za siri.
HISTORIA YA MLALAMIKAJI
Mlalamikaji ni kati ya watoto mapacha waliozaliwa jijini Mwanza na mama ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Mama wa mtoto huyo (kwa sasa ni
marehemu pamoja na mume wake) akiwa muumini wa Kanisa la Evangelical
Assemblies of God (EAGT) aliamua kumtoa mtoto mmoja kwa mama mzazi wa
Flora Mbasha kwa lengo la kumlea, wakati huo mtoto huyo alikuwa na
miezi mitatu.
Ikaelezwa kuwa, mama wa Flora
alikaa na mtoto huyo akimsomesha hadi alipofika darasa la saba ambapo
alimkabidhi kwa Flora na kuishi naye hadi alipofikwa na janga hilo.
Maelezo zaidi yanasema Mbasha
aliweza kufanya kitendo hicho kwa sababu mkewe (Flora) ameondoka
nyumbani na kwenda kuishi hotelini kwa kile kilichodaiwa kwamba kuna
ugomvi mkubwa ndani ya ndoa yao.
Taarifa zaidi zinadai kwa sasa
Mbasha naye hayupo nyumbani kwake huku mlalamikaji yuko Hospitali ya
Amana akiendelea kufanyiwa uchunguzi wa kiafya ili kubaini kama ana
maambukizi ya magonjwa ya zinaa au la!
Kwa upande wake mlalamikaji huyo
alipopigiwa simu juzi kwa lengo la kuthibitisha kuhusiana na
sakata hilo alikiri na kusema amekwishatoa taarifa polisi kwa
kitendo alichofanyiwa na mwenye nyumba huyo huyo.
No comments:
Post a Comment