MASTAA mbalimbali nchini wakiwemo wanamuziki wanatarajiwa kushiriki kwenye tukio maalum la kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ , litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nyumbani Park (Samaki samaki Spot) , Kihonda Morogoro mjini Juni 28.
Akizungumza na mtandao huu , Mratibu Mtendaji wa tamasha
hilo, Kareeem Omary ‘KO’ alisema maandalizi ya tukio hilo litakalokuwa
la kila mwaka, limepwa jina la ‘Love Concert -
Kumbukumbu ya kifo cha Albert Mangwe’.
Kareem, aliwaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuunga mkono
kwenye tukio hilo kwani litakuwa la kipekee na la aina yake ambalo pia litatoa fursa kwa wakazi hao pia
mikoa jirani na watu kutoka nje ya Tannzania ambao watauzulia.
“Nawaomba wadau kujitokeza kuonesha upendo
wa pamoja. Kumbukumbu kwa mpendwa
wetu kama ilivyo utamaduni wetu.” alisema Kareem.
Na kuongeza kuwa, siku hiyo
Watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa pamoja na mama mzazi wa Mangwea kama kumbukumbu.
Kareem aliwataja wasanii watakaotoa burundani, ni
pamoja na kutoka kwa kundi la Wanachemba
ambalo pia aliwahi kuwa nalo marehemu Ngwair,
JSqueezer, P Funky Majani na Mswaki. Kwa upande wa wasanii kutoka
Morogoro ni pamoja na Afande Sele, Team Racers, Mc Koba Chris wa Marya, Belle
9, Samir, Zombie, President Mirrow,
Jordan wa Dejavu na wengine wengi.
Katika siku hiyo ya Juni 28, ambayo ndiyo siku aliyopatwa na
umati marehemu, Kareem alisema kabla ya matukio ya shoo ukumbini, itatanguliwa
na ibada mbili maalum ikiwemo ya
Kanisani na ile ya nyumbani.
Aidha, Kareem alisema
katika tukio hilo, ambalo linatarajia kuanza majira ya jioni ya saa 10 hadi saa
12 jioni, wametoa fursa kwa watoto kutoa burudani ikiwemo ya kuimba na nyinginezo na baadae usiku wa kuanzia saa 2 hadi majogoo
wasanii hao mbalimbali watatawala jukwaa na burudani ya nguvu ya kumbukumbu.
Marehemu ‘Ngwair’ alifariki dunia akiwa nchini Afrika kusini, alijizolea umaarufu kwa nyimbo kama Mikasi na Nisikilize Mi
na nyingine nyingi alizowahi shirikishwa na wasanii mbalimbali nchini wakiwemo
Professa Jay, Nuru, TID, Chidi Benz na wengine
wengi.
No comments:
Post a Comment