Maria Said mama mkubwa wa Nasra, katikati
ni baba mzazi wa Nasra, Rashidi Mvungi, na kulia ni mume wa Mariam Said
wakiwa katika ofisi za ustwawi wa jamii mjini Morogoro baada ya
kukamatwa na kufikishwa polisi kwa tuhuma za kumficha mtoto huyo ndani
ya box kwa miaka 4 baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia kwa
ugonjwa wa malaria .
Muuguzi katika Wodi ya watoto hospitali ya
rufaa ya Morogoro akimuhudumia mtoto Nasra Said mara baada ya
kufikishwa hopsitalini hapo kupatiwa matibabu.
Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.
Habari zaidi soma hapo chini.
MUME na mke wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumficha mtoto kwa miaka 4 ndani ya Box .
Kamanda
wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema tukio hilo lilibainika
Mei 20 mwaka huu majira ya saa 4.45 Asubuhi katika eneo la mtaa
Azimio kata ya Kiwanje Ndege Morogoro.
Alisema
majirani walizingira nyumba ya mwanamke ajulikanae kwa jina la Maria
Said na kutaka kuvunja ndipo polisi walipopata tarifa na kufika katika
nyumba hiyo na kukuta mtoto huyo akiwa katika box.
Alimtaja
mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Nasra Rashid Mvungi mine na nusu
ambapo polisi ilichukua jukumu la kupeleka kesi hiyo Ustawi wa jamii
ili kuendela nayo.
Afisa
Ustawi wa jamii katika ofisi ya mkoa wa Morogoro Oswing Ngungamtitu
alisema mtoto huyo alipelekwa hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa
sababu alionekana kuwa na afya dhoofu.
Alisema
alilazwa na kwamba kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii
huku wakiwachukulia hatua za kisheria walezi wa mtoto huyo Mariam Said
na Mume wake Mtonga Omari.
Baba
mzazi wa mtoto huyo alisema yeye ana mke na watato wengine wa ndoa na
kwamba hakuwahi kumwambia mkewe kama ana mtoto wa nje hivyo ilikuwa
vigumu kumchukua mtoto huyo na ndipo alipomkabidhi mama mkubwa wa mtoto
huyo.
Alisema
kila mara alikuwa akifika kumwona mtoto mama huyo alimwambia mtoto
kalala na hivyo kushindwa kumwona na kujua hali halisi hadi siku ya
tukio na kwamba alikuwa akimpatia matumizi ya mtoto huyo.
Ofisa
mtendaji wa kata hiyo Dia Zongo alisema akiwa katika kazi za kawaida
katika Mtaa wa Azimio, alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanamke
huyo, alimficha mtoto Nasra ndani ya boksi na kwamba hamfanyii usafi
wala kumtoa nje.
Zongo
alisema baada ya kupata taarifa hizo, alimtafuta Mwenyekiti wa mtaa
huo, Tatu Mgagala na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kuanza
kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika na kushindwa
kueleza ukweli juu ya kuwepo kwa mtoto huyo.
Zongo alisema
wakati mtuhumiwa akiendelea kujibu maswali, ghafla mtoto huyo alipiga
chafya na kuanza kukohoa hali iliyowapa wasiwasi na kuamua kuingia
chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasrah akiwa ndani
ya boksi nyuma ya mlango .
Ofisa
mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto huyo kutoka ndani ya nyumba
ya mama yake huyo mkubwa, ghafla kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo
na mawe, walianza kumshambulia mwanamke huyo, kitendo kilichomlazimisha
(mtendaji) kutoa taarifa polisi.
Baada
ya kufikishwa katika kituo cha polisi mwanamke huyo alikiri kuanza
kumlea mtoto huyo tangu akiwa akiwa na umri wa miezi tisa na kwamba
hatua hiyo ilikuja baada ya mama yake, kufariki dunia mwaka 2010.
Mtuhumiwa
huyo alisema kwa mara ya mwisho, alimuogesha mtoto huyo Julai mwaka
jana na kwamba alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi
lililokuwa limewekwa nyuma ya mlango wa chumba cha mwanamke huyo.
Hores Isaack Msaky Dk Mshauri wa watoto katika hospitali ya mkoa wa
Morogoro alikiri kumpokea mtoto huyo na kwamba tayari ameshaanzishiwa
matibabu ya awali .
‘’ Tulimfanyia vipimo vya awali mtoto amebainika kuwa na Nimoni pamoja na utapia mlo na sasa ameshaanza matibabu’’ Alisema
Alisema bado wanaendela na vipimo vingine vya XRay kubaini mtoto huyo alipata ulemavu kwa kupigwa au alizaliwa hivyo.
Alisema
mtoto huyo anamaumivu makali sehemu ya mgongo na mikono na kwamba mwili
wake pia ni mteke kama wa mtoto mchanga hali inayowafanya kuendela
kumfanyia uchunguzi wa kina zaidi.
Baadi
ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mama wa mtoto huyo alifariki
dunia miaka mine iliopita na kwamba Mariamu Ni mama mkubwa wa mtoto
huyo.
Hata
hivyo majirani hao walidai wanahusisha tukio hilo na imani za
kishirikina kutokana na kwamba mama huyo anaakili timamu na analea
watoto wake vema tofauti na mtoto huyo.
No comments:
Post a Comment