Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Sunday, May 18, 2014

BISHA AINGIA MATATANI KUHUSIANA NA FILAMU YA ZENA NA BETINA


MWANADADA Salma Jabu Nisha alizungumzia suala la kuchimbwa mkwara mzito na Gazeti La Sani kwa kuambiwa alipe fedha taslimu za kitanzania Shilingi milioni 100 iwapo anataka kuendelea kuyatumia majina hayo ya Zena NA Betina au laa sivyo atashtakiwa na

Gazeti hilo.

 Nisha alisema: Jamani navyoelewa katika sheria ya jamhuri ya muungano watanzania ya mwaka 1971 ibara ya pili kifungu 'A' kuhusu matumizi ya majina ina sema kila mtu anahaki ya kutumia jina lolote alipendalo mradi awe amepewa na wazazi au kurithi, 

Majina hayo ni ,A' MAJINA YA ASILI, mfano Mwajuma, Amina,Zena, Hamis, Kabuti n.k, Kupitia sheria hii ndio maana unakuta majina hufanana..


  Swali je wenye majina yao kweli hao wa kina zena wakiamua washtaki gazeti la sani kwa kuwafananisha na katuni wanaweza kuwalipa zena wote Tanzania ?....


Hakuwa na mengi ya kusema Nisha bebe bali alimalizia kwa kusema kuwa mashabiki wake wakae mkao wakula ZENA na BETINA zimesalia siku kumi na mbili iwasili madukani kote.

No comments: